Home Kitaifa OFISI YA WAZIRI MKUU KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA

OFISI YA WAZIRI MKUU KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA

Na: Mwandishi Wetu – MWANZA

Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Hifadhi ya Jamii itashiriki katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha ambayo kitaifa yatafanyika Mkoani Mwanza, kuanzia Novemba 21 hadi 26, 2022.

Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamwaja akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.

Hayo ameeleza Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Bw. Omary Mziya wakati wa mkutano na waandishi wa Habari akizungumzia ushiriki wa ofisi hiyo pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo NSSF, PSSSF na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) katika maadhimisho hayo.

Ameeleza kuwa katika wiki ya huduma za fedha wataalamu na maafisa wenye uzoefu kwenye sekta ya hifadhi ya jamii watatoa elimu kwa wananchi ili waweze kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu sekta hiyo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Bw. Omary Mziya (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ushiriki wa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa yanayotarajiwa kuanza rasmi tarehe 21 hadi 26, Novemba, 2022, mkoani Mwanza.

“Sekta ya Hifadhi ya Jamii tumejipanga vyema kutoa kutoa elimu na huduma kwa wananchi, hivyo tunawakaribisha wajitokeze kwa wingi ili tuweze kujenga uelewa wa pamoja kuhusu sekta ya hifadhi ya jamii,” amesema

Akizungumza awali, Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamwaja amewataka wananchi jijini Mwanza na wale wanaoishi karibu na mkoa huo kujitokeza kwa wingi ili kupata uelewa na kuwajengea weledi katika matumizi sahihi ya huduma za fedha zinazotolewa nchini kwa lengo la kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa, katika maadhimisho hayo Mabenki, kampuni za Bima, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Taasisi za Elimu na Utafiti, Watoa huduma kuhusu masuala ya masoko na dhamana, Taasisi za fedha, Wahirika wa Maendeleo, wasimamizi wa Sekta ya Fedha, Wakala wa Serikali, Vyama vya Wafanyakazi, Washirika wa Maendeleo, watoa huduma za fedha, Vyama vya Wafanyakazi na Vyama vya Sekta ya Fedha.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha mwaka huu 2022 yataongozwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ya Fedha kwa Maendeleo ya Watu.”

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!