Home Kitaifa MRADI WA MAJI WA KITELEWASI-LUNDAMATWE WAENDELEA KUWA FARAJA KWA WANANCHI WA KILOLO,MKOANI...

MRADI WA MAJI WA KITELEWASI-LUNDAMATWE WAENDELEA KUWA FARAJA KWA WANANCHI WA KILOLO,MKOANI IRINGA.

Mradi huu wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 788 zilizotoka Mfuko wa Taifa wa Maji (National Water Fund – NWF) umemaliza kero ya muda mrefu ya wakazi 4,667 wa vijiji va Kitelewasi na Lundamatwe ya ukosefu wa majisafi na salama.

Mradi huu ambao kazi yake ilifanywa na mkandarasi FESA Building & Civili Construction ni miongoni mwa miradi ambayo utekelezaji wake ulikuwa umekwama kutokana na changamoto mbalimbali.

Mradi huu ulikamilika na kuzinduliwa mwaka 2019 baada ya kupatikana kwa fedha kutoka Mfuko wa Maji, unaendelea kutoa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi pamoja na mifugo.

Mpaka sasa nyumba 163 zimeshaungiwa huduma ya majisafi na salama ukiacha huduma ya maji inayotolewa kwenye vituo vya kuchotea maji vya jumuiya.

Chombo cha Watoa Huduma ya
Maji cha Kitelewasi-Lundamatwe (KILU) ambacho kinasimamia mradi huo, kimeshakusanya kiasi cha zaidi ya Shilingi 1,171,000 kama makusanyo yanayotokana na huduma inayotolewa kwa wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!