Home Kitaifa RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN ANATARAJIWA...

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN ANATARAJIWA KUFUNGUA MKUTANO WA WANAWAKE NA VIJANA KATIKA BIASHARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kesho septemba 13, 2022 anatarajiwa kufungua Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara la Afrika (African Continental Free Trade Area-AfCFTA Secretariat) utafanyika kuanzia Septemba 12 hadi Septemba 14, 2022 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo Septemba 11, 2022 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uwekezaji, Viwnada na Biashara, Dkt.Ashatu Kijaji akiwa ameambatana na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya AfCFTA Wamkele Mene wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Aesema Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa rasmi Septemba 12, 2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mhamasishaji wa Wanawake na Vijana katika Biashara Barani Afrika kupitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika

Pia amesema Mkutano huo utafungwa rasmi Septemba 14, 2022 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Amesema, mkutano huo unalenga kuwakutanisha pamoja wanawake na vijana katika biashara kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika biashara.

Mheshimiwa Waziri Dkt.Kijaji amesema, hii ni hatua ya kuwawezesha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika biashara na katika mchakato wa kuanzisha Itifaki ya Wanawake na Vijana katika Biashara inayoandaliwa na Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara la Afrika kwa kushirikiana na nchi wanachama wa AfCFTA.

Amesema, mkutano huo wa siku tatu utaongozwa na kauli mbiu isemayo Wanawake na Vijana: Injini ya ya Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika “Women and Youth: The Engine of AfCFTA Trade in Africa’’. Kauli mbiu ambayo inafafanua kwa usahihi jukumu kuu la wanawake katika Afrika na Uchumi wa Dunia na umuhimu wa kuwawezesha wanawake na vijana kushiriki na kutumia ipasavyo fursa za biashara katika AFCFTA Eneo Huru la Biashara la Afrika

Mkutano huo pia unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki wapatao 500 ambao ni pamoja na viongozi mbalimbali wanawake katika ngazi ya marais, marais wastaafu, makamu wa rais, mawaziri wakuu.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA), Wamikele Mene amesema, wanajisikia faraja kuufanya mkutano huo Tanzania kwa lengo la kuwawezesha wanawake na vijana kujiajiri na kutumia fursa za biashara za AfCFTA.

Kukutana kwetu Dar si kuzungumza tu, bali ni kuchukua hatua na kuhakikisha kuwa bara zima linaelewa kuwa iwapo AfCFTA haitafanya kazi kwa wanawake, SMEs, wajasiriamali vijana: hatutafanikiwa.” Amesema Wamukele

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!