Home Kitaifa MHANDISI MANYANYA AIMWAGIA SIFA RUWASA

MHANDISI MANYANYA AIMWAGIA SIFA RUWASA

Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mkoani Ruvuma Meshimiwa Mhandisi Stella Manyanya aimeisifia RUWASA kwakutatua kero za uhaba wa maji jimboni Nyasa na maeneo mengi ya nchi.

Mheshimiwa Manyanya alisema hayo kwenye ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement KIVEGALO na wataalamu wake mkoani Ruvuma alipotembelea miradi mbalimbali ya maji vijijini.

Leo ziara ya Mkurugenzi Mkuu ilitembelea Wilaya ya Nyasa katika mradi wa maji wa Lituhi Group wenye thamani ya shilingi 6,595,019,723 ambao ukikamilika utahudumia wananchi wapatao 14,186.

Kazi zinazofanyika katika mradi huo ni Ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye mita za ujazo (500M3), Ujenzi wa vituo vya kuchotea maji kumi na tisa, Ujenzi wa chanzo katika mto Lukali, Ununuzi wa bomba zenye urefu wa mita 77,570, Uchimbaji wa mitaro, ulazaji wa bomba pamoja na ufukiaji umbali wa mita 77,570. 6 pamoja na Ujenzi wa ofisi ya chombo cha watumiaji maji.

Pia Wilayani Nyasa ziara ya Mhandisi KIVEGALO ilitembelea mradi wa maji wa Liuli group wenye thamani ya shilingi 4,718,087,448.

Mradi huu unahusisha Ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji yenye mita za ujazo M3 (100, 135, 300), Ujenzi wa vituo vya kuchotea maji kumi na tisa (19 DPs), Ujenzi wa chanzo kimoja katika mto Nkalachi, Ununuzi wa bomba zenye urefu wa mita 49,750, Uchimbaji wa mitaro, ulazaji wa bomba pamoja na ufukiaji umbali wa mita 49,750 na Ujenzi wa ofisi ya chombo cha watumiaji maji.

Mradi huu ukikamilika utahudumia vijiji vitano vyenye idadi ya watu wqpatao 15,823.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!