Home Kitaifa MBUNGE WA JIMBO LA KINONDONI MHE. ABBAS TARIMBA AKABIDHI KADI ZA BIMA...

MBUNGE WA JIMBO LA KINONDONI MHE. ABBAS TARIMBA AKABIDHI KADI ZA BIMA YA AFYA KWA WAJUMBE ZAIDI YA 603

NA ABRAHAM NRAMBARA

MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni (CCM) wilayani Kinondoni Mkoani Dar es Salaam Abbas Tarimba amekabidhi Kadi za Bima ya Afya kwa Wajumbe zaidi ya 603 wa Chama Cha Mapinduzi wa jimboni kwake.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi Kadi hizo iliyofanyika leo Septemba 11, 2022 jimboni humo, Tarimba amesema amefanya hivyo kutokana na umuhimu wao lengo likiwa ni kuwafanya wawe na uhakika wa maisha yao.

Nidhahiri kwa mwitikio huu, Wanakinondoni jambo hili wamelipokea vizuri na wanalifurahia. Viongozi wengi wakipata nafasi, husahau waliokuwa nao, si mnaona wengi, na wengine hawasaidii mpaka wapate nafasi, hivyo mimi nimepata nguvu sana kutokana na matendo mazuri ya Rais Samia,” amesema Tarimba.

Amesema kwamba kiongozi anatakiwa kuwa mtu wa mfano, ambapo ameeleza kuwa pamoja na figisu anazofanyiwa hatatingishika hata siku moja.

Nataka niwaambie hili suala la bima ya afya limeleta mazungumzo mengi sana katika makundi mbalimbali katika Kata yetu. Tulivyolianzisha wengine wakapeleka figisu figisu juu likasimamishwa, nilivyolianzisha Makumbusho, wakasemba kwamba nafanya kampeni,” amesema Tarimba na kuongeza kuwa,

Jamani mimi sipigiwi kura na Wajumbe na Wenyeviti wa Mashina, lakini nimeweka siasa kando nimeangalia utu. Nimeangaliwa kwamba katika Katiba yetu ya Chama cha Mapinduzi kiongozi wa kwanza anayetajwa ni mabalozi,“.

Amesema kwamba mabalozi wengi ni watu wa zima japo kwa sasa wameanza kuingia vijana, hivyo kuna busara, akili, uzoefu na mazingatio katika watu hao.

Ameongeza kuwa viongozi hao wamekuwa wakipata changamoto nyingi ikiwemo za kutatua migogoro ya wananchi hata nyakati za usiku.

Hivyo kutokana na kazi yao kuwa nyeti na ya muhimu na utu uzima wao na mazingira wanayoishi ameamua kuwakabidhi kadi hizo lengo wawe na uhakika wa maisha yao.

Alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhurui ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa na Wanakinondoni katika kuwaletea maendeleo na kwamba hajawasahau.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!