Home Kitaifa MAONESHO YA 17 YA VYUO VIKUU; RUAHA CATHOLIC UNIVERSITY WAJA NA TEKNOLOJIA...

MAONESHO YA 17 YA VYUO VIKUU; RUAHA CATHOLIC UNIVERSITY WAJA NA TEKNOLOJIA MPYA

Na Magreth Mbinga

Chuo cha Ruaha Catholic University (RUCU) kimekuja na kozi mbili za kompyuta sayansi katika maonesho ya vyuo vikuu sabato yanaandaliwa na TCU katika uwanja wa Mnazi mmoja.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa kozi za shahada na zisizo za shahada katika chuo cha RUCU Dkt Willy Migodela na kusema kuwa wanafunzi wametengeneza mashine ambayo itafungwa kwenye gari, mashine ya juisi na yakufukuza mbu.

Wanafunzi wetu wametengeneza mashine ambayo ina uwezo wa kudhibiti uzito mkubwa kwenye magari ambapo gari litabeba mzigo mkubwa gari halitawaka na litatoa mlio wa tahadhali (alarm)mpaka mzigo utakapo punguzwa, mashine ya juisi ambayo itasaidia mteja kujihudumia endapo ataweka sarafu yake itatoa juisi kulingana na kiasi cha pesa yake na wametengeneza mashine ya umeme ambayo inasaidia kufukuza mbu ndani itasaidia Serikali katika vita ya kupambana na malaria” amesema Dk Migodela.

Aidha Dk Migodela amesema Chuo chao kina kozi mbalimbali kama vile Afya, Sheria, Ualimu ,Biashara na Kompyuta sayansi zote zinatambulika na TCU lakini wana mitaala ambayo wameiandaa kama kozi nyingi ambazo zinamuandaa mwanafunzi kujiajiri .

Mfano katika kozi za Afya kuna pharmacy, laboratory na Environmental science sambamba na hizo tunakozi ambayo inamuandaa mwanafunzi kuwa mtafiti na utafiti huo ni katika magonjwa na kutibu kwa madawa ya asili wametengeneza dawa ya fangasi na ugonjwa wa ngozi na zinafanya vizuri lakini bado hazijapitishwa na mamlaka husika “amesema Dkt. Migodela

Sanjari na hayo Dkt Migodela amesema wana kozi za muda mfupi kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu na amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao chuo cha Ruaha Catholic University (RUCU) kwani hatajuta sababu atapata taaluma pia kuna mazingira mazuri ya kusoma vilevile hawabagui dini japo kuwa chuo ni cha kanisa katoliki lakini ndani ya chuo hiko kuna msikiti kwa ajili ya wanafunzi wa kiislamu kufanya ibada.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!