Home Kitaifa WATUMISHI WA WILAYA YA TEMEKE WAMPONGEZA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA...

WATUMISHI WA WILAYA YA TEMEKE WAMPONGEZA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUPANDISHA MADARAJA NA ONGEZEKO LA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA.

Na Mwandishi wetu.

Leo Tarehe 03/08/2022 baadhi ya watumishi wa kada mbalimbali kutoka katika Wilaya ya Temeke wamezungumza na waandishi wa habari na kupongeza juhudi mbalimbali za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tangu ameingia madarakani.

Wakizungumza na waandishi wa habari wamesema Rais Samia amejipambanua kuwa anawajali watumishi sana na kwa kuzingatia maslahi yao na alianza kwa kuwaondolea kadhia ya watumishi wenye deni la mkopo wa elimu ya juu, “Rais Samia alipoingia madarakani alifuta penati hii na imeleta ahueeni kubwa na Sasa Deni linalipika, baada ya mabadiliko hayo aliyekuwa analipa milioni 8 Sasa analipa milioni 4 pekee.

Kwa upande wa posho na nauli wamesema Rais Samia ameongeza kiwango kwa asilimia 100 na hii imeleta ahueni kubwa sana kwa watumishi wanapopewa kazi maalumu.

Kuhusu suala la nyongeza ya asilimia 23 sisi watumishi tumelielewa sana mana lengo kuu Rais Samia amezingatia kuboresha Hali za kiuchumi za watumishi wa kiwango cha chini ambao ni wengi zaidi katika kada mbalimbali za utumishi wa umma, hapa amezingatia wenye viwango vidogo vya mishahara.

Watumishi hao wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi , ubora na kiwango cha Hali ya juu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!