Home Kitaifa JESHI LA POLISI LAFANIKIWA KUONDOA KERO YA PANYA ROAD MTAA WA BUGURUNI...

JESHI LA POLISI LAFANIKIWA KUONDOA KERO YA PANYA ROAD MTAA WA BUGURUNI KISIWANI

Na Magreth Mbinga

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mh Omary Kumbilamoto amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuweza kurudisha hali ya utulivu ambayo ilipotea kwa muda mrefu Mtaa wa Buguruni Kisiwani(Ghana) iliyokuwa ikisababishwa na wahalifu hasa panya road ambapo wananchi walikuwa wakiishi kwa wasiwasi.

Pongezi hizo amezitoa wakati akihutubia Wananchi wa Mtaa wa Kisiwani katika mkutano ulioandaliwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo na kusema kuwa vijana ambao walikuwa wanasumbua katika eneo hilo wamedhibitiwa na sasa Wananchi wanaweza kutembea na kuishi kwa amani .

“Kipekee niwashukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Amos Makala pamoja na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Jumanne Murilo kwakweli wamefanya kazi kubwa sana ilifikia mahala ndugu zetu Waislam walikuwa hawawezi kwenda kuswali swala ya alfajiri kwasababu ya kuhofia na Wakristo vilevile walikuwa hawawezi kuwahi ibada ya asubuhi sababu ya kuhifia usalama wao” amesema Mh Kumbilamoto.

Pia Diwani wa Kata ya Buguruni Mh Busoro Pazi amewataka wananchi kutengeneza mazingira ya usalama majumbani kwa kuweka taa nje ya nyumba ambayo itasaidia ulinzi kuweza kumulika mazingira ya nyumba yake.

Mwenyekiti ,Mtendaji wa Mtaa pamoja na Makamanda wa ulinzi shirikishi tusaidiane kuzibaini nyumba zote ambazo hazijawekwa taa nje kwaajili ya usalama ziweze kuwekwa mara moja kwaajili ya kuhakikisha usalama na kuondoa giza” amesema Mh Pazi.

Aidha Mwenyekiti wa Mtaa huo Mh Uwesu Bakari amewataka wazazi kushirikiana na jeahi la polisi endapo mzazi atabaini mtoto wake amekamatwa kwa tuhuma za uhalifi aweze kumuacha kwanza ajifinze maadili na sio kukimbilia kumtolea zamana ambapo wakirudi mtaani wanarudia sababu hawajakaa kwa muda mrefu ili abadilishe tabia.

“Namshukuru sana Polisi Kata vijiwe vyote hapa anaingia lakini mtu akikamatwa dakika mbili mzazi anaenda kituoni kwenda kumtoa kwa kufanya hivi Jeahi la Polisi munalivunja nguvu muache akae asiyefinzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu” amesema Mh Uwesu.

Sanjari na hayo Mtendaji wa Mtaa wa Kisiwani Bwana Azizi Shididi amesema wanajua jitihada wanazozifanya Jeshi la Polisi katika kupambana na panya road kwa hivyo wanalipongeza sana kupitia Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Wambura.

“Licha ya jitihada hizi za jeahi la Polisi tinatambua kuna watu wanafanya mikakati ya kulikatisha tamaa jeshi shidi ya hatua zake zinazochukua katika kuwakabili panya road kama Wananchi wa Buguruni Kisiwani tunaomba lisikatishwe tamaa kwakuwa wengi wanaobeza hili zoezi sio wahanga wa panya road” amesema Mh Shididi.

Vilevile Mwananchi wa Mtaa huo wa Kisiwani aliejitambulisha kwa jina la Prisca Masanja amepongeza Serikali na Jeshi la Polisi kwa kuweza kuleta amani katika Mtaa huo na kusema kuwa wale panya road ni wauwaji na kuwataka wazazi ambao wamewaficha watoto wao ndani wawasalimishe kituo cha Polisi .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!