Home Kitaifa ELIMU YA KISHERIA NA USURUHISHI IWE KIPAUMBELE KWA WANANCHI “RC MTAMBI”

ELIMU YA KISHERIA NA USURUHISHI IWE KIPAUMBELE KWA WANANCHI “RC MTAMBI”

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amesisitiza elimu ya kisheria na usuruhishi ipewe kipaumbele na kutolewa kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa kwa niaba yake leo Februari 3 na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka kwenye maadhimisho ya kilele cha wiki na siku ya Sheria nchini.

Akitoa salam za serikali amesema elimu ni suala la muhimu wananchj kuipata ili kuweza kuwa na ufahamu wa kisheria na kuepukana na migogoro mbalimbali.

Amesema wananchi wakiwa na elimu itakuwa rahisi kukaa katika meza ya usuruhishi na kufikia makubaliano bila kuingia kwenye Mahakama.

RC Mtambi amesema serikali inaendelea kutatua migogoro ili kuipunguzia mashauri Mahakama na kuendelea kuwa na ufanisi kwenye utendaji.

” Mimi kama mkuu wa Wilaya kwenye ofisi yangu nimetenga siku ya kuwasikiliza wananchi na yanapokuja masuala ya kisheria tunashirikiana na wadau kuyasikiliza.

” Serikali ipo tayari kushirikiana na Mahakama hususani katika eneo la usuruhishi wa migogoro inapotufikia kabla ya kufika kwa wananchi”amesema.

Mwenyekiti wa Chama wa Wanasheria wa Tanganyika ( TLS) Onyango Otieno amesema kuelekea Dira ya Taifa ya 2050 wana taaluma wamejikita katika utatuzi wa migogoro.

Amesema TLS wataendelea kutoa msaada wa kisheria kwa kuwa ni kinara wa ushauri kwa serikali katika uchechemuzi wa kisheria kwa kuwa huwezi kutoa msaada wa kisheria bila wanasheria.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Fahamu Mtulya ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye siku hiyo ya Sheria amesema jazi ya Mahakama ni kutenda haki na ndio dhumuni kubwa kama sala na dua zilizotolewa na viongozi wa dini.

Amesema Mahakama ni chombo cha wananchi kinachofanya kazi kutokana na kodi zao na hata Dira ya Taifa ya 2050 inasisitiza kuzingatia haki na utu wa mtu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!