Home Kitaifa WASIRA ATOA WITO KWA VIONGOZI WA CCM KUWASIKILIZA WATU KWENYE MAENEO YAO

WASIRA ATOA WITO KWA VIONGOZI WA CCM KUWASIKILIZA WATU KWENYE MAENEO YAO

Na Shomari Binda-Musoma

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Taifa Stephene Wasira ametoa wito kwa viongozi wa chama hicho kuwasikiliza watu kwenye maeneo yao.

Kauli hiyo ameitoa leo februari 3 mjini Musoma ikiwa ni muendelezo wa ziara yake inayoendelea mkoani Mara.

Amesema kusikilizwa kwa watu na kutatua matatizo yao ni siraha kubwa kwa chama ambacho kinashika dola na kinaendelea na mipango ya kuendelea kushika dola.

Wasira amesema kŵenye eneo la uvuvi,kilimo,ufugaji na maeneo mengine wapo watu ambao wanapaswa kusikilizwa na viongozi wa chama.

Amesema watu katika maeneo hayo wakisikilizwa na kutatua matatizo yao wataendelea kukipenda chama na kukipa nafasi ya kuendelea kushika dola.

Wasira amesema wapo vijana ambao wanapaswa kusikilizwa na hiyo ni kazi ambayo inapaswa kufanywa na viongozi wa CCM.

Akizungumzia suala la uchumi wa mkoa wa Mara Wasira amesema licha ya viwanda kufungwa vikiwemo vya samaki kutokana na uhaba wa samaki na jitihada zitafanywa ili kuboreshwa kwa hali ya uchumi.

Amesema baada ya kuchaguliwa kama Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa na kutoa salamu zake kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa katika shukrani zake alielezea namna ya chama kuendelea kushika dola.

” Musoma nawapongeza na kuwashukuru kwa mapokezi makubwa mliyonipa nami nawaahidi sito waangusha na tuko pamoja.

” Wito wangu kwa nchi nzima ni kuwataka viongozi wa CCM kuwasikiliza watu kwenye maeneo yenu na kutatua matatizo yao”,amesema.

Akizungumza mbele ya Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema ilani imetekelezwa vyema jimboni na eneo linalohitaji kuimalishwa ni uchumi wa wananchi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma mjini Magiri Benedicto amesema maelekezo yaliyotolewa kuhusu kuwasikiliza watu watayafanyia kazi.

Amesema chama kitaleta wagombea wanaokubalika katika nafasi za udiwani na ubunge na kuahidi kura za kishindo kwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!