Home Kitaifa CHAMA CHA WAHASIBU KUWAJENGEA UWEZO MACHINGA

CHAMA CHA WAHASIBU KUWAJENGEA UWEZO MACHINGA

Mapema leo Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum wameingia makubaliano ya kuwawezesha wafanya biashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga kwa lengo la kuwajengea uwezo.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalum Mhe Amon Mpanju ambapo chama hiko kitawajengea uwezo wafanya biashara ndogo ndogo wa kujisimamia kifedha na kukua .

Pia Mhe. Mpanju amesema hiyo ni fursa kwa wamachinga waitumie vizuri wakati wakisubiria Serikali inakuja na sheria ya Wafanya biashara ndogo ndogo.

“Tunahitaji TAA waingie watusaidie ili tupate kanzidata zilizo sahihi ambazo zitasaidia kuwawekea mazingira rafiki wafanya biashara ndogo ndogo “amesema Mpanju.

Sanjari na hayo Mwenyekiti wa SHIUMA Taifa Ernest Matondo amesema ushirikiano ambayo wanaingia na TAA yawasaidie kufanikisha shughuli zao za kimachinga na Wizara ibadilishe Sheria ili Viongozi wa Machinga wapate mamlaka ambazo halmashauri wanazo.

Aidha Makamu mwenyekiti TAA Victorious Kamuntu amesema makubaliano hayo yanalenga namna gani makundi maalumu watawezeshwa na wadau mbalimbali kukuza biashara zao.

“Huu mradi unalenga watu wa chini kabisa namna gani watakuza biashara na uchumi wa nchi, sisi tunaangalia sera na kushauri Serikali ili SHIUMA wakue wafike juu ” amesema Kamuntu.

Vile vile Mwanasheria wa Serikali Tabitha Dida amesema TAA ina madhumuni ya kujengea uwezo wafanya biashara ndogo ndogo pande zote mbili zimeingia makubaliano ili kukuza biashara za Machinga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!