Home Kitaifa BINGWA FESTIVAL KUFAIDISHA MOJA KWA MOJA WANAFUNZI WA VYUO

BINGWA FESTIVAL KUFAIDISHA MOJA KWA MOJA WANAFUNZI WA VYUO

Na Magreth Mbinga

Tamasha la Bingwa festival ni Maalum kwaajili ya kuleta burudani ya kusherehekea na kuangalia mechi za kombe la dunia ambalo limeandaliwa na Famous Entertainment na kudhaminiwa na HISENSE pamoja na TIGER ROYALTY.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mkuu wa Famous Entertainment Chrisostome Millambo na kusema kuwa tamasha hilo limegawanyika katika sehemu mbili ya Kwanza ni compus festival ambapo watazunguka katika vyuo vikuu vya hapa Dar es Salaam na kuonesha mechi za kombe la Dunia na itafanyika katika mzunguko wa 16 na kutakuwa na matukio maalumu ikiwemo kuangalia mechi za nusu fainali sambamba na mechi ya fainali ambayo wataangalia Palm Village.

“HISENSE na TIGER LOYALTY ndio washirika wetu wakubwa ambao wamewezesha hili jambo kwenda kuwafikia vijana na jambo kubwa ambalo tutalifanya compus tour ni fursa ambazo vijana wanaweza kuzipata kwenye kombe la Dunia na michezo kwa ujuma”amesema Millambo.

Pia Millambo amesema watakapo kuwa vyuoni washirika wao wote watapata fursa ya kukutana na wanafunzi sambamba ikiwa pamoja na kuongea nao kutakuwa na mabonanza .

Aidha Afisa Masoko ya kampuni ya HISENSE Joseph Mavula amesema kampuni yao ndio mdhamini Mkuu wa kampeni hiyo waliona ni nafasi nzuri kushiriki wakiwa kama wadhamini wakuu wa kombe la Dunia ili kuweza kuonyesha mashindano mubashara katika maeneo ya wazi hususa ni vyuoni.

“Kutakuwa na tukio kubwa ukiachana na hii ambayo tutaanza kuonyesha hatua ya 16 bora tutaweza kuonyesha pia hatua ya fainali pale Palm Village ambapo siku hiyo tutatoa zawadi ya televisheni ya Nchi 55 ambayo ni HD 4K”amesema Mavula.

Sanjari na hayo Mkurugenzi TIGER ROYALTY Pius Matonya amewataka watu hasa wanafunzi wa vyuo ambao watashiriki bingwa festival kupakua TIGER ROYALTY ili kufanya malipo na endapo watalipia pesa watapata faida ya asilimia 5 .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!