Na Theophilida Felician Kagera.
Timu ya Mpira wa miguu JKT QUEENS imetwaa kikombe cha ubingwa wa mashindano ya CECAFA mwaka wa 2023 yaliyokuwayakifanyika Nchini Uganda.
Timu hiyo imefanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa magori 5-4 dhidi ya timu ya CBE ya Ethiopia ambapo waliishinda kwenye kipindi cha penati baada ya wote kutoka sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 za mchezo.

Akizungumzia juu ya ushindi huo baada yakupokelewa na timu ya uongozi wa Mkoa Kagera pamoja na wananchi kwa ujumla eneo la kata ya Rwamishenye Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera
kocha Mkuu Esitha Chaburuma amesema kuwa mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika viwanja vya FUFA Njeru mjini Kampala nchini Uganda hayakuwa mepesi kwani kila mmoja alikuwa akihitaji kuibuka na ushindi wa nchi yake japo wao kutokana na jinsi walivyokuwa wamejipanga vizuri wamejikuta wakiibuka kidedea dhidi ya wenzao.
“Kwanza ni mshukuru mwenzi Mungu tulimaliza mashindano yetu salama kwa maana tuliwahidi watanzania wenzetu tunaenda kupambana nasiyo kushiriki nakweli tumepambana hatimaye tumeludi na matokeo ya ubingwa” kocha Esitha akizungumza mbele ya wananchi .
Esitha licha ya ubingwa huo ameahidi kwamba JKT QUEENS bado inamategemeo makubwa ya kufanya yaliyomazuri zaidi kwenye mashindano hayo ukanda wa Afrika yatakayofanyika nchini Ivory coast.
Ameongeza kuwa wakiwa Nchini Uganda walipata uungwaji mkono vya kutosha kutoka kwa watanzania walioko huko chini ya ubalozi wa Tanzania uliofanya jitihada za kuwaunga pamoja watanzania hatimaye wakawa bega kwa bega na timu hiyo.
Amewashukuru wananchi wa Kagera na uongozi wake kwa ujumla kwa jinsi walivyowaonyesha mapokezi makubwa baada ya kuwasili mjini Bukoba hii Leo Tarehe 31 Agost 2023.
Kwa upande wake kaimu katibu tawala wa Mkoa Kagera kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Fatma Mwassa Projestus Rubanzibwa akiipokea kwa bashasha na furaha isiyokifani timu hiyo ameipongeza kwa namna ilivyojitahidi kupambana katika mashindano hayo yaliyozishirikisha timu mbalimbali za Afrika mashariki hatimaye kuleta heshima kubwa ya ushindi nchini.
Amewaombea mafanikio mema zaidi katika mashindano hayo hayo kwa upande wa Afrika yatakayo fanyika nchini Ivory coast.
Ikumbukwe kuwa Mnamo Tarehe 11 Agost mwaka huu tumu hiyo iliondoka hapa mkoani Kagera kuelekea Uganda kwenye mashindano hayo na kurejea kwake nchini leo tarahe 31 Agost 2023.









