Akizungumza Noely Salinge Laizer ambae ni Afisa Mauzo na mwakilishi wa kampuni ya Palijati katika Maonesho ya Nanenane yanaendelea katika maeneo ya Nyamongoro Mwanza Tanzania amesema Kampuni ya Palijati imejipanga kuhakikisha inauza Dawa za viatilufu lakini pia na kutoa Elimu na kujifunza kwa Vitendo namna Dawa mbalimbali za kampuni hio ya Palijati inavyofanya kazi.
Noely amesema Kampuni hiyo ipo kwa ajili ya kuwasaidia wakulima na kuwashauri kuacha kulima kilimo cha Mlaazoea lakini pia nakuomba wakazi wa Kanda ya Ziwa kutumia Maonesho haya ya Nane Nane kuwa Fursa Kwa Wakuliwa hivyo wanatakiwa kutumia Maonesho haya ya Nane Nane ili kuweza kuwafungulia Fursa wakulima.
Lakini pia Focus Laulant Mkulima aliyetembia eneo ilo wanapouzia Viwatilifu na kutolea Elimu ameshukuru kampuni hiii kuwa imefungua kimawazo na kifikra alisema Mama huyu “Nilikuwa nalima lakini sikuwa na uelewa wa kutosha kuhusu kilimo baada ya Kutembelea kampuni hii ya Palijati “
“Nimepata uelewa wa kutosha hivyo naenda kuleta mabadiliko makubwa kwenye kilimo” alisema Baba huyo
Hata hivyo kilimo ndiyo njia pekee ya kupata fedha tofauti na sehemu nyingine lakini pia amewaomba Vijana kujitokeza Kwa wingi ili kupata Elimu ya kilimo na kutolalamika nq kusema kuwa kuna Changamoto ya Ajira.
Alisema Watanzania wengi wanaishia kulalimika hali ni ngumu wanashindwa kujikita kwenye Kilimo na Serikali inawekeza fedha nyingi sana kwenye kilimo hivyo tuchangamkie Fursa hiyo ya kilimo kwani ndio suluhisho ya Matatizo ya ajira.









