Home Kitaifa WIZARA YA FEDHA YASISITIZA ELIMU YA FEDHA KUKUZA UCHUMI WA NCHI IFIKAPO...

WIZARA YA FEDHA YASISITIZA ELIMU YA FEDHA KUKUZA UCHUMI WA NCHI IFIKAPO 2050.

Na. Saidina Msangi na Asia Singano, WF, Dar es Salaam.

Wizara ya Fedha imebainisha kuwa imeelekeza bajeti yake katika kumwezesha mwananchi kiuchumi, ikilenga kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Mwaka 2050 kupitia kuimarisha sekta binafsi, kukuza elimu ya juu, na kuongeza uelewa wa masuala ya fedha na kodi kwa umma.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde, wakati akizungumza na vyombo vya habari, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Munde alisema Maonesho ya mwaka huu yameonesha mafanikio makubwa katika matumizi ya mifumo ya kidijitali na maboresho ya huduma, mambo ambayo ni nguzo muhimu katika kusogeza huduma za kifedha karibu zaidi na jamii na kurahisisha shughuli za kiuchumi nchini.

“Wizara ya Fedha imeweka mkazo mkubwa katika kuongeza pato la Taifa na pato la mtu mmoja mmoja kama msingi muhimu wa maendeleo endelevu, ikiwa ni pamoja na kufikia uchumi wenye thamani ya dola trilioni moja na pato la mtu mmoja mmoja kufikia dola 7,000 ifikapo mwaka 2050,” alisema Mhe. Munde

Aidha, Mhe. Munde aliwahimiza wananchi kuachana na mifumo ya fedha isiyo rasmi na badala yake watumie taasisi rasmi za kifedha katika shughuli zao za kila siku, hatua inayolenga kuongeza usalama wa fedha zao, uwazi, na kuleta ufanisi wa jumla katika mifumo ya kifedha nchini.

Alisema Wizara pamoja na Taasisi zake inaendelea kutoa elimu ya huduma za fedha pamoja na elimu ya kodi kwa wananchi waliotembelea maonesho hayo waweze kuepuka mikopo isiyo rasmi ijulikanayo kama mikopo umiza ili kuendana kikamilifu na mikakati ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050.

‘’ Kuna umuhimu wa kuendelea kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma za fedha ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi, jambo linalotazamiwa kuwa chachu ya ongezeko la pato la mwananchi mmoja mmoja na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa, alisisitiza Mhe. Munde.

Mhe. Munde alipongeza Wizara pamoja na Taasisi zake kwa hatua kubwa zilizofikiwa katika utoaji wa elimu kwa wananchi katika maonesho hayo na kusisitiza kuendelea kufanya maboresho ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa bora zinazokidhi mahitaji ya wananchi kwa ufanisi na kuchangia moja kwa moja katika kukuza pato la Taifa.

Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania”, ni maonesho ya 50 toka kuanza kwake ambapo yanaambatana na kuadhimisha miaka 50 ya maonesho hayo.

MWISHO.

CAPTIONS.

PIX 1

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akizungumza na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo walioshiriki kutoa elimu kwa umma, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania”, yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

PIX 2

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akimsikiliza Meneja wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (Hazina Saccos), Bw. Festo Mwaipaja akieleza kuhusu utendaji wa chama hicho, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania”, yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

PIX 3

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akioneshwa moja ya machapisho ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), na Mkuu wa Chuo hicho Prof. Hozen Mayaya, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania”, yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua.

PIX 4

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akimsikiliza Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikali (GPSA), Bw. Peter Mayila, akieleza majukumu ya wakala, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasab ni Fahari ya Tanzania”, yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

PIX 5

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akimsikiliza Afisa Tehama Mwandamizi, Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Bw. Goodluck Luhanjo, akieleza majukumu ya Taasisi hiyo, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasab ni Fahari ya Tanzania”, yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

PIX 6.

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mipango Fedha na Utawala, Prof. Jeremia Makindara, akieleza majukumu ya chuo hicho, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasab ni Fahari ya Tanzania”, yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

PIX 7

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Masoko, Mfuko wa SELF, Bw. Petro Mattaba, akieleza majukumu ya Mfuko wa SELF, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasab ni Fahari ya Tanzania”, yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

PIX 8

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Prof. Hozen Mayaya (kulia), wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasab ni Fahari ya Tanzania”, yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

PIX 9

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Shamim Mdee na watumishi wengine wa Bodi hiyo, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania”, yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

PIX 10

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua, wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha wanaoshiriki kutoa Elimu katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania”, yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

11.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Denis Simba, akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha ambao wanashiriki kutoa Elimu katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania”, yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!