Home Kitaifa TADB YAWAWEZESHA WAFUGAJI WADOGO ZAIDI YA 92, 000 KUPITIA MRADI WA MAZIWA...

TADB YAWAWEZESHA WAFUGAJI WADOGO ZAIDI YA 92, 000 KUPITIA MRADI WA MAZIWA WA TI3P

Jumla ya wafugaji wadogo 92,831 na wadau wa mnyororo wa thamani wa maziwawa Tanzania Bara na Visiwani-Zanzibar wamenufaika na Mradi Shirikishi waWasindikaji na Wazalishaji wa Maziwa (TI3P) tangu ulipoanzishwa mwezi Machi mwaka 2022, ambapo asilimia 30 ya wanufaika hao ni wanawake.

Mradi huo wa miaka minne unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya KilimoTanzania – TADB pamoja na Bill & Melinda Gates Foundation huku ukitekelezwakwa kushirikiana na Heifer International, Land O’Lakes Venture37 pamoja naTanager.

Akiongea wakati wa Maonesho ya Wiki ya Maziwa Mkoani Iringa, Mratibu waMradi wa TI3P, Joseph Mabula amesema mradi huo unalenga kutatua changamotombali mbali zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ndogo ya maziwa ilikuongeza uzalishaji, na kuboresha kipato cha wafugaji wadogo wa maziwa nchinihuku akiishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. SamiaSuluhu Hassan kwa kuipa uzito mkubwa sekta ndogo ya maziwa.

Mabula amesema tangu kuanza kwake, mradi umewezesha utolewaji wa mikopowa Zaidi ya shilingi bilioni 42 kwenye sekta ndogo ya maziwa ikiwalenga wasindikaji wa maziwa, wafugaji, wasambazaji wa pembejeo, pamoja na wadauwengine kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya maziwa.

Fedha hizo zimewezesha uanzishwaji wa viwanda vipya vya kuchakata maziwapamoja na upanuzi na maboresho kwa jumla ya viwanda 17 vya usindikajivimefikiwa kwa uwekezaji wenye thamani ya shilingi bilioni 22.8.

Aidha, mradi umewezesha ununuzi wa mitamba 3,330 yenye thamani ya zaidi yashilingi bilioni 11.09, hatua iliyochangia kuongeza uzalishaji na tija katika sekta yamaziwa nchini.

Kupitia mradi huo, wafugaji wameendelea kupata huduma za ugani, pembejeobora, masoko, pamoja na huduma za kifedha kwa ajili ya uwekezaji katika sektandogo ya maziwa, jumla ya wasindikaji 19 wa maziwa wamenufaika na programuza kuongeza uwezo, huduma za ugani, na ufanisi katika uzalishaji.

Katika kuhamasisha ushirikishwaji wa kijinsia na ukuaji jumuishi, TADB ilitoaruzuku linganifu yenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 kwa wafugaji wadogo 1,216, wakiwemo wanawake 397, ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa mitambabora, uzalishaji, uchakataji na uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa maziwa.

Vilevile, biashara tano (5) zinazomilikiwa na wanawake zilipatiwa mitambo yakuchemshia maziwa yenye thamani ya shilingi milioni 75 ili kuongeza fursa za masoko kwa wafugaji. Wasindikaji wanawake watano (5) walinufaika na ruzuku za TI3P, huku wasindikaji 12 wakipata ruzuku maalum za kuchochea usawa wakijinsia katika biashara zao.

Katika kuboresha ukusanyaji na kuhakikisha ubora wa maziwa, mradiumefanikiwa kuanzisha na kuimarisha vyama vya ushirikia/msingi 45 pamoja navikundi mbalimbali vya wafugaji na wafanyabiashara kwenye seta ndogo yamaziwa. Vikundi hivyo kwa sasa vinakusanya zaidi ya lita 25,664 za maziwa kwasiku,hivyo kuchochea upatikanaji wa maziwa hususani kwa viwanda nawachakataji wadogo wa maziwa.

Mratibu wa Mradi huo, amesema kuwa mradi umefanikiwa kuanzisha vituo 23 vyaukusanyaji wa maziwa nchini kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 1.157 kwakushirikiana na wadau mbalimbali, ikiwemo vyama vya ushirika, wafugaji, wasindikaji wa maziwa, na washirika katika utekelezaji wa mradi.

Mabula amehihimisha kwa kusema kuwa mradi huo unaendelea kushughulikiachangamoto za kisera na kisheria zinazoathiri ukuaji wa sekta ndogo ya maziwasambamba na kuzingatia masuala mtambuka kama usawa wa kijinsia na lishe bora kwa maendeleo endelevu ya sekta hiyo.

Ametoa wito kwa wadau wote kuendelea kushirikiana katika kutatua changamotozinazoikabili sekta ndogo ya maziwa na kutumia kikamilifu fursa zinazotolewakupitia mradi wa TI3P pamoja na huduma za TADB.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!