Home Kitaifa JK AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMUAGA JACKSON ISDORY UDSM

JK AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMUAGA JACKSON ISDORY UDSM

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Viongozi wa Serikali, wanataaluma na jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wameungana kumuaga Jackson Isdory Mushi, aliyefariki kwa ajali ya gari mkoani Mbeya, huku wakimkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika kujenga taswira na mahusiano ya taasisi hiyo.

Jakaya Mrisho Kikwete ambaye Rais Mstaafu ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ameongoza mamia ya waombolezaji katika shughuli hiyo.

Katika shughuli hiyo ya maombolezo walihudhuria viongozi mbalimbali wengine ni Spika wa Bunge Mstaafu, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye, walioambatana na viongozi wengine wa chuo hicho.

Waombolezaji na watu mbalimbali wamemkumbuka marehemu kwa nidhamu, utu na weledi wake kazini, wakisema aliacha alama ya kipekee katika utumishi na mahusiano ya kijamii ndani ya chuo na nje yake.

Jackson Isdory Mushi anatarajiwa kuzikwa Jumanne, Juni 2, 2026 katika kijiji cha Usseri, wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!