Home Kitaifa KAFULILA KUONGOZA MDAHALO WA UBIA WA UMMA NA BINAFSI SUA

KAFULILA KUONGOZA MDAHALO WA UBIA WA UMMA NA BINAFSI SUA

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP-Centre), imeandaa Mhadhara wa Umma utakaotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa PPP-CENTRE,  David Kafulila, siku ya Ijumaa, Julai 17, 2026.

Mhadhara huo unatarajiwa kujadili mada juu ya “Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi kama chachu ya mageuzi ya kilimo katika utekelezaji wa Mpango wa Nne wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.”

Tukio hili litafanyika  Kampasi Kuu ya SUA, Morogoro, likiwalenga Wanafunzi, Wataalamu, wadau wa kilimo pamoja na Wananchi wenye nia ya kujifunza nafasi ya ubia wa sekta ya umma na binafsi katika kuharakisha maendeleo ya sekta ya kilimo na uchumi wa taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!