


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepokea kitabu maalum chenye habari za picha kutoka kwa Mkurugenzi wa Tahsil Solutions, Bw. Benny Kisaka. Kitabu hicho kina mkusanyiko wa taarifa za kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar mwaka 2025.
Dkt. Mwinyi amempongeza Mkurugenzi huyo kwa ubora na umakini uliotumika katika kukusanya taarifa na kutengeneza kitabu hicho.
Mkurugenzi wa Tahsil Solutions, Bw. Benny Kisaka, amewasili Ikulu Zanzibar leo, tarehe 20 Novemba 2025, kwa ajili ya kumkabidhi Rais Dkt. Mwinyi kitabu hicho, ambacho baadaye kitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.








