Home Kitaifa ZOEZI LA SENSA ASILIMIA 93.45 ZA KAYA ZILIZOHESABIWA

ZOEZI LA SENSA ASILIMIA 93.45 ZA KAYA ZILIZOHESABIWA

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe.Anna Makinda akizungumza na Waandishi wa habari leo Agosti 29,2022 wakati akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa zoezi ambalo lilitakiwa kuisha leo.

Na Magrethy Katengu

Zoezi la Sensa kuanzia 23hadi 29 Agosti mwaka huu limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufikia asilimia kaya 93.45% zimehesabiwa huku asilimia 6.55% bado hawajahesabiwa hesabu za asubuhi ya saambili asubuhi .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutoa taarifa hiyo Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Anna Makinda amesema zoezi la kuhesabu watu linatarajiwa kukamilika hii leo lakini kwa wananchi ambao bado hawajahesabiwa wafike katika ofisi za serikali ya mtaa au kupiga simu namba 0753-665491au 0626-141515 ,0784665404,0656279424 kutoa taarifa zao kwa karani wa sensa na atawafikia kuwahesabu na zoezi hilo litadumu kwa siku saba kuazia Agosti 30-5

Ameongeza kuwa ifikapo agosti 30-1 Septemba kutakuwa na zoezi la sensa ya majengo yote ikiwa ni pamoja na ofisi ili kuipa nafasi serikali kuboresha sera yake ya makazi hivyo ametumia fursa hiyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa kwa kutoa taarifa sahihi.

Wananchi ambao hajahesabiwa hakikisheni licha ya kuachiwa fomu za kujaza mtumie fursa hii kwa kupiga simu kwani waratubu na makarani wote wako kazini muhesabiwe ni kwa faida yenu na nchi kiujumla nafasi bado ipo“amesema Kamisaa
Kwa faida

Naye, mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu katika Ofisi za Taifa ya Takwimu Emilian Karugendo amesema makarani wa vijijini ndiyo waliopewa power benk kwa ajili ya Vishikwambi vyao kutokana na changamoto ya baadhi ya maeneo yao bado umeme haujafikiwa wanaofanya maeneo ya mijini wao umeme upo kila mahali na tumekuwa tukiwapigia tanesco kama kuna hitilafu ya umeme.

Aidha vinavyotumika katika shughuli ya sensa baada ya kazi hiyo vitatumika kwa mpango Maalumu wa kiserikali huku akiwotoa hofu Makarani wote watalipwa malipo yao baada ya kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!