Home Kitaifa ZAIDI YA SHILINGI MILIONI MIA TANO (500) ZIMEKUSANYWA UPITIA HALMASHAURI NA MABARAZA...

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI MIA TANO (500) ZIMEKUSANYWA UPITIA HALMASHAURI NA MABARAZA YA MIJI

Zaidi ya shilingi Milioni mia tano (500) zimekusanywa kupitia halmashauri na mabaraza ya miji kwa ajili ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mikopo nafuu isiyo na Riba.

Ameyasema hayo Waziri wa Nchi Afisi ya Rais – Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan wakati akijibu suali la Mhe Zaina Abdallah Salum Mwakilishi Nafasi za Wananwake kuhusu fedha zinazokusaywa kupitia halmshauri na mabaraza ya miji kwa ajili ya kuyawezesha makundi maalum, katika kikao cha tisa cha Baraza la Kumi la wawakilishi huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar

Amesema fedha hadi kufikia tarehe 31 Agosti, 2022, jumla ya shilingi 551,324,144 zimekusanywa kutoka Halmashauri na Mabaraza ya Miji/Manispaa Unguja na Pemba kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali ambapo utaratibu unaotumika utahakikisha kuwa fedha hizi zinawafikia na kuwanufaisha walengwa waliokusudiwa kwa kuweka miongozo ya namna ya utoaji wa mikopo hiyo ambapo majina ya vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu yataandaliwa kupitia Halmashauri na Mabaraza ya Manispaa husika na watapatiwa fomu za mikopo kupitia Afisi za Wakuu wa Wilaya.

Aidha Waziri Soraga amesema katika kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa mujibu wa malengo yaliyowekwa afisi yake itahakikisha inafanyakazi kwa karibu kwa kushirikiana na taasisi nyingine husika kwa ajili ya kujiridhisha kwa kuyatathmini maombi yaliowasilishwa ili kuona miradi iliyoombwa inatekelezeka na kuleta tija kwa waombaji wa mikopo hiyo.

”Watendaji wa ARKUU kwa kushirikiana na watendaji wa Halmashauri husika watashirikiana katika kuyatathmini maombi yaliyowasilishwa ili kujiridhisha kuwa miradi iliyoombwa inatekelezeka na kuleta tija, lakini pia kuhakikisha kuwa kiwango kilichoombwa kinalingana na aina ya biashara iliyoombewa mkopo huo.” Alisema Soraga

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!