Home Kitaifa YUHOMA EDUCATION LIMITED INATOA USHAURI KUENDANA NA SOKO LA AJIRA

YUHOMA EDUCATION LIMITED INATOA USHAURI KUENDANA NA SOKO LA AJIRA

Na Magreth Mbinga

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya YUHOMA EDUCATION LIMITED Yusuph Yahaya ambayo inashughulika na utoaji wa ushauri wa elimu kwa wanafunzi wasome nini,wasome wapi ili kuendana na soko la ajira la nchini Tanzania.

Amezengumza hayo Julai 20 katika maonesho ya 17 ambayo yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu ,Sayansi na Teknolojia ( TCU ) na kusema kuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa amesema waandae vijana kuendana na soko la ajila.

Mimi kama mdau wa elimu ninatamani sana wanafunzi wapewe ushauri waweze kusoma kozi gani ambazo zinahitajika eidha hapa kwetu Tanzania au popote Duniani ili waweze kupunguza changamoto kubwa ya msongamano wa swala la ajira” amesema Yusuph.

Pia Yusuph ameishukuru TCU kwa kuandaa maonesho hayo ya Vyuo Vikuu Tanzania amegundua ni sehemu muhimu sana wadau wote wanakuja ,wanajua watapata taarifa mbalimbali za Vyuo Vikuu na namna ya kujiunga.

Sanjari na hayo Yusuph amesema Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu kwa usimamizi wa Wizara ya Elimu wamepewa mamlaka mawakala na kutambuliwa ambao wanaweza kuonesha jinsi gani mwanafunzi anakwenda .

Changamoto zipo za aina tatu ambazo ni changamoto za wazazi ambapo wazazi wengi uelewa wao unakua mdogo kwenye swala la kusoma nje na ukizingatia tokea limeibuka hili gonjwa la virusi vya UVIKO 19 pamoja na vita ambayo inaendelea sababu Tanzania ni sehemu ya Dunia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!