Home Kitaifa WIZARA YA MAJI YAJA NA MATANKI YA MAJI YA PLASTIKI

WIZARA YA MAJI YAJA NA MATANKI YA MAJI YA PLASTIKI

Chamwino, Dodoma

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji kwenye kata ya Dabalo Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma, ambapo ametoa pongezi nyingi kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini(RUWASA)na kwa Kampuni ya PLASCO inayotengeneza matanki makubwa ya plastiki yaliyotumiwa katika mradi huo.

Aidha Mhe.Aweso amesema hii kwa mara ya kwanza inatumika katika miradi ya maji hapa Nchini,na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kuitumia teknolojia hiyo badala ya Ile ya kujenga kwani inatumia muda mfupi wa wiki mbili tu kuyaweka katika chanzo cha Maji, na yanadumu kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka 60.

Mradi huo unaghalimu zaidi ya shilingi Milioni 907,unatekelezwa na RUWASA chini ya ofisi ya Meneja wa Mkoa wa wa Dodoma na Wilaya ya Chamwino kwa fedha za mfuko wa Taifa wa maji, na mkandarasi anayeujenga ni Medes Company Ltd na unatarajiwa kuhudumia wakazi 8,134, utakapokamilika Julai 30,2022.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!