Home Kitaifa WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI YA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA...

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI YA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 06, 2022 ameweka jiwe la msingi ya ujenzi wa jengo la utawala katika halmashauri ya Wilaya ya Singida, ambalo ujenzi wake unategemea kukamilika ifikapo Novemba, 2022.

Ujenzi wa jengo hilo utakaogharimu shilingi Bilioni 2.7 hadi kukamilika kwake, unajengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza umefikia hatua ya umaliziaji sawa na asilimia 92 na awamu ya pili umefikia hatua ya ujenzi wa ghorofa ya kwanza sawa na asilimia 45.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Singida Ester Chaula kuisimamia idara ya manunuzi ili mjenzi aweze kukamilisha ujenzi huo kwa wakati, “Mjenzi asisumbuliwe, ili aweze kukamilisha ujenzi huu, idara ya manunuzi nunueni vitu kwa bei halisi

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la ujenzi wa majengo ya halmashauri zote zisizo na majengo.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Singida Nusrat Hanje amewataka wakazi wa mkoa wa Singida kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika kuhakikisha anailetea nchi maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!