Home Kitaifa WAZIRI MKENDA AZINDUA TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU

WAZIRI MKENDA AZINDUA TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU

Na Magrethy Katengu

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adlof Mkenda amesema hali ya uchapaji na usambazaji wa vitabu inaukai sana hivyo Serikali kuanzia mwakani itatenga bajeti ya bilioni moja Ili kunusuru kwa kununua vitabu vya ithibati na kuvipeleka mashuleni ili kuleta hamasa .

Ameyasema hayo leo katika Uzinduzi wa tuzo ya Taifa Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambapo amesema kupitia tuzo hiyo wanafungua ukurasa wa kuchochea ari mpya ambapo mwakani serikali itatenga fedha ya bilioni moja ya kusimamia vitabu vya ithibati serikali kuingie sokoni kwa kuvinunua na kuvisambaza mashuleni.

“Tumetenga kwenye bajeti kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuhakikisha tunaanzia kutekeleza mapendekezo ya wadau wetu na taratibu zote zitafanyika chini ya TET lengo ni kukidhi matakwa ya wadau kuchangamsha soko siyo kushuhudia baadhi ya taasisi za uchapashaji zinafungwa “amesema Mkenda

Hata hivyo amesema Mwandishi atakayepata tunzo watahakikisha kitabu chake kinachapwa na kununua kisha kukisambaza kuanzia mashuleni hadi maktaba ya Taifa Ili kumsaidia kufidia gharama zake alizotumia.

Kwa upande wake alizotumia Kamishna Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Lyabwene Mutahaba amewasisitiza Waandishi wa vitabu kuandika kuhusu watoto kwani wamekuwa wakipitia changamoto mazingira magumu kwa kufanyiwa vitendo viovu ndani ya Jamii na wahusika ni ndugu zao wa karibu vitendo hivyo ni pamoja ikiwemo kulawitiwa kubakwa,kupigwa,kunyanyapaliwa hivyo wakiandika vitabu itasaidia kubadilisha Jamii

” watoto ni tunu kubwa tuliyopewa na Mwenyezi Mungu kuwa baraka lakini Leo tukiwaangalia baadhi ya watoto wanavyoteseka kutokana na changamoto wanazokutana nazo machozi yananitoka kila nikisoma magazieti visa na Mikasa yao ni vya kutisha kalamu yenu itwaokoa
Tutaendelea kushirikiana Ili kuboresha Ari ya usomaji wa vitabu

Naye Penina Mrama Mwenyekiti tuzo ya Taifa Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu amesema Mbunifu atakayeshiriki atatakiwa kuandika nyanja Moja tu Kwa mada atakayoichagua yaani Riwaya au ushairi na andiko liwe makini litakalojikita katika masuala ya Kijamii na dirisha ya kuwasilisha kutakuwa wazi kuanzia Septemba 13- Novemba 30 mwaka huu

Aidha majaji watapiti maandiko ya kila mshiriki atakayetuma kupitia barua pepe na Zawadi nono Kwa washindi itakuwepo ambapo mshindi wa kwanza atapewa kiasi cha shilingi milioni 10 huku wa pili akipatiwa shilingi milioni 7 na watatu alipewa milioni 5 hivyo Waandishi wote wa vitabu andikeni kazi nzuri na hii itakuwa kila mwaka .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!