Home Michezo WAZIRI MCHENGERWA AJIUNGA RASMI NA KLABU YA JESHI LUGALO GOFU

WAZIRI MCHENGERWA AJIUNGA RASMI NA KLABU YA JESHI LUGALO GOFU

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa amekabidhiwa rasmi kadi ya uwanachama wa Klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Gofu na kuanza Mazoezi ya Mchezo huo kwa mara ya kwanza.

Akizungumza mara baada ya kumaliza mazoezi katika klabu hiyo Waziri Mchengerwa amesema, amevutiwa na mchezo huo ikiwa ni sehemu moja ya mazoezi na ajira hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kuucheza Mchezo huo pamoja na Michezo mengine.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema,Mh Waziri ameonesha umahiri mkubwa wa kuucheza Mchezo wa Gofu huku akiwaomba viongozi mbalimbali na Watanzania kujifunza Mchezo huo.

Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa kushoto kwake Mwenyekiti wa Klabu ya lugalo gofu Brigedia jenerali Mstaafu Michael Luwongo kushoto kwake Nahodha wa klabu hiyo Meja Japhet Masai maara baada ya kumkaribisha rasmi kujiunga na Klabu hiyo Jijini Dar es salaam

Naye Mkufunzi wa Klabu hiyo Geoffrey Levirian amesema,Ingawa ni mara ya kwanza kwa Waziri Mchengerwa kucheza Mchezo wa Gofu na ameshangwazwa na kiwango alichokionesha Wakati akifanya mazoezi.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa pia amesaini fomu ya kujiunga na Klabu hiyo na kukabidhiwa kitabu Cha sheria za Mchezo wa Gofu na Nahodha wa klabu ya Lugalo Meja Japhet Masai.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa akikabidhiwa vitabu vya mafunzo na Nahodha wa klabu ya Lugalo gofu Meja Japhet Masai Mara baada ya kujiunga rasmi na uanachama wa Klabu hiyo Jijini Dar es salaam

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!