Home Kitaifa AWESO AMUONDOA MENEJA WA RUWASA KARAGWE KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA MIRADI YA MAJI.

AWESO AMUONDOA MENEJA WA RUWASA KARAGWE KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA MIRADI YA MAJI.

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amemsimamisha Kazi Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijini RUWASA wilaya Karagwe, Mhandisi Magai Kakuru kwa kushindwa kusimamia miradi ya Maji inayoendelea kutekelezwa Wilayani Karagwe na kusababisha wananchi wa maeneo mbalimbali kushindwa kupata huduma ya maji.

Ametoa agizo hilo leo septemba 11, 2022 wakati wa ziara yake ya siku Moja wilayani Karagwe mkoani Kagera na kukagua mradi wa Maji wa Chanika/Omululama ulipo wilayani humo na kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa kukagua mradi wa maji wa

Mhandisi huyu anajitahidi kufanya kazi na amefanya mengi lakini haiendani na kasi inayohitajika kwahiyo ataenda kusaidia kwenye kazi nyingi, hapa karagwe nitaleta Meneja Mwingine anayeendana na kasi tunayoitaka” amesema Aweso

Waziri Aweso amesema wilaya ya karagwe imekuwa ikisumbuliwa na miradi mingi kichefuchefu ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa haitoi huduma ya maji kwa wananchi.

Aidha, Aweso ameagiza kuondolewa Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa vijijini nane wilayani Karagwe na mchakato wa kumpata Mkandarasi Mwenye Uwezo na atakayetekeleza miradi ya maji ndani ya muda wa mkataba.

Waziri Aweso amesema Serikali hatamvumilia wala kumbembeleza Mhandisi yeyote atakayeshindwa kusimamia miradi ya maji na akawasisitiza kusimamia na kukwamua miradi ya maji, “faraja ya Mhandisi wa Maji ni kuona Wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama na yenye kutosheleza”.

Nae, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amesema Kiu ya Wananchi wa wilaya ya karagwe ni kuona miradi ya maji inakamilika na wanapata maji safi na salama.

Bashungwa ameongeza kuwa kuanza kuanza kutekelezwa kwa mradi wa Maji Rwakajunju umeibua matumaini makubwa kwa wananchi wa Karagwe ambao wamekuwa wakihangaika kwa kipindi kirefu kupata Maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!