Home Kitaifa WAZIRI MASAUNI AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA USHAURI BIASHARA YA KABONI.

WAZIRI MASAUNI AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA USHAURI BIASHARA YA KABONI.

Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

WAZIRI Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Masauni ameeleza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza majukumu yake katika kusimamia masuala ya mabadiliko ya tabianchi na biashara ya Kaboni kwa mbinu zilizo bora na zenye maslahi kwa Taifa na Kimataifa.

Waziri Masauni ameyasema hayo wakati Akizungumza na Wanahabari Jijini Dodoma leo Machi 10,2025 katika Uzinduzi wa Kamati hiyo itakayoshughulikia masuala ya biashara ya Kaboni hapa Nchini.

“Napenda kusema kuwa kama Serikali tutaendelea kuhakikisha kwamba tunatekeleza majukumu yetu katika kusimamia masuala ya mabadiliko ya tabianchi na biashara ya kaboni kwa kutumia mbinu bora na zinazozingatia maslahi ya Taifa na Kimataifa“.

Aidha ameikumbusha Kamati hiyo jukumu lake kuu kuwa ni pamoja na Kufanya tathmini na kutoa mapendekezo kuhusu njia bora na mwenendo wa biashara ya Kaboni nchini sambamba na kubaini na kuchambua changamoto za mfumo mzima wa biashara ya kaboni nchini kuanzia kwenye usajili, upimaji, uuzaji na makubaliano ili kuongeza uwazi na ufanisi na uwajibikaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!