Home Kitaifa WANANCHI, WATUMISHI MUHEZA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KILIO CHA TOZO NA KUSHUKA BEI...

WANANCHI, WATUMISHI MUHEZA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KILIO CHA TOZO NA KUSHUKA BEI MAFUTA.

NA BONIFACE GIDEON, MUHEZA

WANANCHI na Watumishi wa Umma Wilayani Muheza Wamemshukuru Rais Samia pamoja na Serikali kwaujumla kwa Matumizi Mazuri ya Fedha za tozo na kushusha Bei za Mafuta ambapo Serikali imeshusha Sh.400 kutokana na Ruzuku ya Bil.100 inayotolewa na Serikali Kila mwezi.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari Wilayani humo , Wamesema Suala la Tozo ni zuri japo linamaumivu kwa Wananchi lakini limesaidia kutekereza Miradi mingi ya Maendeleo ndani ya Muda mfupi ikiwamo Ujenzi wa Miradi ya Kimkakati ambayo ni Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere na Reli ya SGR.

Akizungumza kwaniaba ya Watumishi wa Serikali Wilaya ya Muheza Bernad Luanda alisema ndani ya Muda mfupi wa Uwepo wa Tozo za Miamala Zaidi ya Vituo vya 234 Nchini vimejengwa vikigharimu Bil.117 ,
Ujenzi huu wa Vituo vya Afya umeenda sambamba na ununuzi wa Vifaa Tiba ambapo zaidi ya Bil.145 pia sambamba na hayo pia Serikali imefanikiwa kujenga Shule mpya za Sekondari 214 kwenye kata ambazo Awali zilikuwa hazina Shule hizo” Alisisitiza Luanda

Aliongeza kuwa katika Sekta hiyo ya Elimu Serikali imefanikiwa kusomesha Wanafunzi wa Elimu ya juu kupitia Bodi ya Mikopo Nchini ambapo Bil.221 zimetumika ,

Kupitia Tozo hizi Watoto wa Maskini wameweza kunufaika kwa kupata Elimu ya juu katika vyuo vikuu Nchini lakini Serikali imefanikiwa kuajiri Watumishi wapya wa Afya 7,612 wakiwemo Madaktari lakini pia na Ujenzi wa Majengo wa Wagonjwa wa nje OPD zikiwamo Maabara na vyumba vya Upasuaji” Alisisitiza Luanda

Alisema wao kama Watumishi Wa Umma Wanaishukuru Kamati kuu ya CCM kupitia kikao kilichoketi hivi karibuni na kufanya tathmini ya Malalamiko ya Wananchi juu ya Makali ya Tozo hizo,

Katika kikao Cha Kamati kuu ya CCM kilichoketi hivi karibuni kiliweza kuishauri Serikali kufanyia kazi Baadhi ya Mambo likiwamo Suala la Tozo na tunaimani kuwa litafanyiwa kazi kwakuwa CCM ndio inayounda Serikali ili kurejelea Ilani ya CCM ya kuwapatia nafuu ya Maisha Wananchi” Alisisitiza Luanda

Nao Baadhi ya Wakazi wa Muheza akiwemo Hilda Barnaba Alisema kupitia Tozo hizo Wilaya hiyo imepata Mabadiliko makubwa ya hususani kwenye Miradi ya Afya na Barabara,

Tunashukuru Sana tunaona tumeongezewa Barabara za lami lakini pia hata kwenye Sekta ya Afya hapa Muheza tumeona Vituo vya Afya na Barabara za lami ndani ya Mji , tunaishukuru Serikali kwakufanikisha Haya Mana na sisi Wilaya yetu imepata Hospitali ya Serikali na imeshaanza kutoa Huduma” Alisisitiza Hilda

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!