Home Kitaifa WANANCHI WA MIPAKANI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA TISHIO LA UGONJWA WA EBOLA

WANANCHI WA MIPAKANI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA TISHIO LA UGONJWA WA EBOLA

Kutoka Kagera 28/9/2022

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ametoa wito kwa wananchi waliopo katika maeneo ya mpakani mwa Uganda na Tanzania kuchukua tahadhari wakati Serikali inaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya tishio la ugonjwa wa Ebola.

Prof. Makubi ametoa wito huo leo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera, baada ya kutuma timu ya wataalam kutoka Wizara ya afya na kukutana na viongozi wa mkoa ili kujionea utayari wa kukabiliana ugonjwa huo uliotokea nchi ya jirani.

Prof. Makubi ameeleza kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola hapa nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!