Home Kitaifa VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA WAHIMIZWA KUSIMAMIA USAFI WA MAZINGIRA ILI KUANGAMIZA...

VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA WAHIMIZWA KUSIMAMIA USAFI WA MAZINGIRA ILI KUANGAMIZA MAZALIA YA MBU NDANI YA JAMII

Na. Catherine Sungura, Tanga

Viongozi wa Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi kufanya usafi wa mazingira kwenye maeneo yao pamoja na kufukia madimbwi yote ili kuteketeza mazalia ya mbu yanayopelekea kuongezeka kwa mbu na ugonjwa wa malaria nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Tanga na Waziri wa Afya Mhe. Ummy wakati akizindua Afua ya unyunyiziaji wa viuadudu vya Kibaiolojia kwenye mazalia ya Mbu kwa Wilaya za Tanga, Handeni na Lushoto iliyofadhiliwa na Serikali ya Uswisi kupiti Shirika la Maendeleo la Uswisi.

e

Amesema licha ya kutekeleza afua hiyo ya unyunyiziaji wa viuwadudu vya kibailojia kwenye mazalia ya mbu bado pia Jamii inahitajika kuboresha usafi wa mazingira kwa kuangamiza mazalia yote ya mbu katika maeneo tunayoishi hivyo basi Viongozi wa Serikali za Mitaa wawajibike katika kuhimiza usafi wa mazingira.

Tukifunika madimbwi itasaidia kuzuia magonjwa yaenezwayo na mbu pamoja na magonjwa mengine kama Dengue,matende na mabusha homa ya bonde la ufa na Chikungunya” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Hata hivyo Waziri Ummy ametaka kutekelezwa kwa usimamizi wa Sheria ya Afya ya Jamii ya Mwaka 2009 na Sheria ya Usimamizi ya Mazingira ya mwaka 2004.

Amesema hatua hiyo ikifanyika kikamilifu, itasaidia kupunguza idadi ya mazalia,kupunguza wingi wa mbu katika maeneo tunayoishi na hatimaye kupunguza maambukizo ya ugonjwa wa Malaria na magonjwa mengine.

Yeyote ambaye hatotekeleza wajibu wake katika kuharibu mazalia ya mbu achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria hizi” amesisitiza Waziri Ummy.

Ugonjwa wa Malaria bado ni tatizo katika nchi yetu, hata hivyo Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya Malaria nchini kati ya watu 100 wanaofika hospitali 10 wana changamoto ya Malaria“Amefafanua Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha,Waziri Ummy amesema mradi huo ambao utakuwa wa miaka miwili utaweza kuleta manufaa yaliyokusudiwa na hivyo kuendelea na afua zingine za udhibiti wa Malaria ikiwemo ya kuwa na mazingira safi.

“Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria inatekeleza mpango mkakati wa Malaria wa miaka mitano unaolenga kupunguza kiwango cha maambukizi ambapo mwaka 2012 kiwango cha Malaria ilikua 14% na kupungua hadi kufikia 7.5% mwaka 2017” amesema Waziri Ummy Mwalimu

Naye, Balozi wa Uswis nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot amesema Wangependa kuiona Tanzania isiyo na Malaria na ndio sababu wamefadhili fedha za kitanzania Bilioni 400 kwa ajili ya kutekeleza afua hiyo kwa kipindi cha miaka miwilli bega kwa bega na Serikali ya Tanzania.

Amesema pamoja na juhudi za Serikali na washirika wake bado Malaria ipo na ina sababisha vifo, hivyo Serikali ya Uswis itaendelea kushirikiana katika afua za kujikinga na kutokomeza Malaria nchini.

Afua ya Unyunyiaji Viuadudu vya Kibailojia kwenye mazalia ya mbu Mkoa wa Tanga itatekelezwa kwenye Wilaya za Tanga,Lushoto na Handeni ambao utekelezaji wa afua hii unafadhiliwa na Serikali ya Uswis kupitia Shirika la Towards Elimination of Malaria ina Tanzania(TEMT-Project)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!