Home Kitaifa TMA YATOA TAHADHARI JUU YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA:

TMA YATOA TAHADHARI JUU YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA:

Na Magrethy Katengu

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imewataka watu wote kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu na ushauri na utabíri unaotolewa na TMA ili kuepuka changamoto zinazoweza

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mtaalamu na Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka kitengo kikuu cha Utabiti Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Rose Senyagwa wakati akizungumzia mvua zinazondelea nchini hususani katika maeneo ya ukanda wa Pwani.

Senyagwa amesema kuwa kuwa mvua zinazoendea katika ukanda huo pamoja na baadhi ya maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki zimesababishwa na upepo wenye unyevuunyevu unaovuma kutoka bahari ya hindi kueleka katika maeneo ya nchi yetu na hivyo kusukuma unyeunyevu huo.

‘Mvua zinazoendelea katika maeneo ya ukanda wa Pwani nikimaanisha Mikoa ya Tanga,Dar es salaam,Pwani,Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro,lindi Mtwara,Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na baadhi ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki mikoa ya Kilimanjaro,Arusha na Manyara zimesababishwa na upepo wenye unyevuunyevu unaovuma kutoka bahari ya hindi’amesema Senyagwa

Amesema mvua hizo zilianza mwezi Juni katika kipindi cha Kipupwe na zimekuwa zikijitokeza kwa mvua za kawaida hivyo wameziita mvua za nje ya msimu na wanatarajia zitaendelea kuwepo katika kipindi cha Mwezi July mpaka Agosti mwaka huu.

Amesema kuwa kutokana na utabiri wa msimu wa kipupwe ambao ulitolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa mwishoni mwa mwezi Mei maeneo mengi ya nchi yalitarajiwa kuwa na vipindi vya baridi na upepo mkali.

Amesema katika maeneo ya ukanda wa Pwani na Maziwa Makuu vipindi vya upepo mkali bado vinatarajiwa kuendelea kujitokeza upepo unaofikia Kilomita 40 au kuzidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofika mita mbili yanatarajiwa kuendelea kujitokeza

Mtaalamu huyo wa Uchambuzi wa Hali ya Hewa amesema ni vyema katika kipindi hicho cha Baridi na Upepo mkali wananchi wakazingatia tahadhari zinazotolewa kwa kujikinga ili kujihadhari na madhara ya kiafya.

‘Aidha nyakati ambazo kuna ukungu mzito barabarani madereva wanapaswa kuwa makini wanapoendesha magari kwani inapunguza uono wa kuoa umbali mrefu hivyo wanashauriwa kuzingatia na kuchukua tahadhari’amesema Senyagwa

Hata hivyo Mamlaka hiyo pia imewashauri wananchi wanaofanbya shughuli zao kuendelea kuchukua tahadhari kipindi cha upepo mkali ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!