Home Kitaifa TANZANIA -UK KUIMARISHA BIASHARA

TANZANIA -UK KUIMARISHA BIASHARA

Na Mercy Maim

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ally Gugu

Kampuni na wafanyabiashara wakubwa 30 kutoka Uingereza wapo nchini kushiriki kongamano la pili la biashara kati ya Tanzania na Uingereza.

Kongamano kama hilo, kwa mara ya kwanza lilifanyika nchini, Novemba mwaka 2021 likizikutanisha kampuni 13 kutoka nchini humo.Akizungumza kuhusu kongamano hilo leo Naibu Katibu Mkuu, Uwekezaji, Viwanda na Biashara, anayeshughulikia uwekezaji, ALLY GUGU amesema masuala ya kisera, sheria na changamoto za biashara na uwekezaji yatajadiliwa.”Ili kuimarisha ushirikiano na uhusiano tumeona tuanzishe kongamano hili ili kujadili masuala ya kisera, fursa na changamoto wanazokitana nazo wafanyabiashara ili zifikishwe kwa mamlaka husika na kutafutwa ufumbuzi,” amesema.

Kwa mujibu wa GUGU, majadiliano yatakayofanyika yatahusisha taasisi za umma za Uingereza na Tanzania, kadhalika wafanyabiashara kutoka Tanzania na Uingereza.Mwisho wa kongamano hilo, amesema mataifa hayo yatajadili kwa pamoja kilichojadiliwa na kutatua kila changamoto.

Balozii wa Uingereza nchini Tanzania, DAVID CONCAR, amesema pamoja na nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU), nchi zinazoendelea zitanufaika na fursa zilizopo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!