Home Kitaifa TAKUKURU PWANI YABAINI UPIGAJI UNAOFANYWA NA WAZABUNI KATIKA BAADHI YA MIRADI YA...

TAKUKURU PWANI YABAINI UPIGAJI UNAOFANYWA NA WAZABUNI KATIKA BAADHI YA MIRADI YA MAENDELEO

Na Magreth Mbinga

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Pwani haina uvumilivu baada ya kubaini Serikali inakosa mapato kutokana na wazabuni kuto kutoa stakabadhi za kielektroniki katika baadhi ya miradi ya maendeleo.

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Kamishna Christopher Myava katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa wataendelea na uchunguzi wa vitendo vya rushwa na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale watakao bainika kutenda makosa.

Tutaendelea kukagua utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo katika Mkoa wa Pwani ili miradi hiyo iweze kutekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa na kwa ubora unaostahili na kuleta tija kwa jamii“amesema Myava.

Pia Myava amesema jumla ya malalamiko 98 yalipokelewa kati ya hayo 42 yalihusu rushwa uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa na malalamiko 56 hayakuhusu rushwa katika malalamiko hayo yasiyohusu rushwa 25 walalamikaji walishauriwa ,malalamiko 11 yalihamishiwa taasisi nyingine na malalamiko 20 yalifungwa baada ya walalamikaji kupata suluhu ya malalamiko yao.

Aidha Myava amesema kuwa katika utekelezaji wa miradi yapo mapungufu yaliyobainika ikiwa ni pamoja na Wazabuni walioleta vifaa vya ujenzi wa kituo cha afya Nyamato Wilaya y a Mkuranga kutotoa stakabadhi za ki elektroniki (EFD) kwa kisingizio cha ubovu wa mashine ambapo Serikali ilikosa mapato kutokana na huduma zilizotolewa na Wazabuni hao.

Katika hili TAKUKURU Mkoa wa Pwani tutaendelea na uchunguzi hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika baada ya uchunguzi kukamilika,pia imebainika kwamba katika mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari mpya ya Shungubweni Wilayani Mkuranga taratibu za manunuzi zilikiukwa katika utoaji wa zabuni “amesema Myava.

Sanjari na hayo Myava amesema TAKUKURU kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama imebainika uwepo wa vifaa vya ujenzi visivyo na ubora katika ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Jibondo Wilayani Mafia ambapo matofali 6,000 hayakukidhi viwango baada ya upimaji wa kitaalamu kufanyika.

Vilevile katika mfumo wa manunuzi ya umma kwenye Idara mbalimbali za Serikali ilibainika taratibu za kuwapata watoa huduma hazikuwa shindanishi na fedha zinazokusanywa zinatumika kabla ya kupelekwa benki na hivyo kukosekana kwa taarifa kamili za nini kilikusanywa ikilinganishwa na kiasi kilichotumika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!