Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameagiza Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kuisajili kwa wakala wa barabara vijijini TARURA barabara ya Kikuyu Mangaliza kuelekea Kijiji cha Kilambo.
“Tujenge misingi imara katika kutekeleza miradi ya maendeleo ili tuimarishe ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, miundo mbinu ya afya na miundo mbinu ya elimu”
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene alipokuwa anazungumza na wananchi wa kata ya Mangaliza katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.