Home Kitaifa SHIRIKA LA RELI TANZANIA LATIA SAINI MKATABA WA UKARABATI WA BEHEWA 20...

SHIRIKA LA RELI TANZANIA LATIA SAINI MKATABA WA UKARABATI WA BEHEWA 20 ZA MIZIGO NA CCTTFA

Shirika la Reli Tanzanian (TRC) linashukuru Serikali kwa kutoa fedha kwaajili ya kutekeleza mradi wa ukarabati wa behewa 200 za mizigo ukarabati huo ni utekelezaji wa mkataba ambao ulisainiwa kati ya TRC na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kukarabati behewa 40 za mizigo yaliyogharimu kiasi cha fedha Shilingi Bilioni moja na Milioni miamoja thelathini na tano.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa na kusema kuwa lengo la mradi huo ni kuipa uwezo TRC katika usafirishaji wa mizigo kwa kutumia reli ya MGR.

Kwa mujibu wa makubaliano haya kazi hii itachukua miezi 24 yakihusisha ununuzi wa vipuli kwaajili ya ukarabati wa behewa 20 za mizigo na zoezi hili litahusisha ubasilishaji wa matumizi ya behewa zilizopata ajali kutoka behewa zilizozibwa yaani (damage covered wagons) kuwa behewa za wazi (flat wagons) “amesema Kadogosa.

Pia Kadogosa amesema hivi sasa kuna miradi mingi ya ujenzi inayoendelea na itakayoanza hivi karibuni katika Nchi ya Tanzania na Nchi jirani ambayo inahitaji usafiri wa uhakika kwaajili ya kusafirisha mitambo mizito ya ujenzi
na vifaa mbalimbali na behewa za wazi (flat wagons) itasaidia kazi hiyo kwa kiasi kikubwa.

Sanjari na hayo kipande cha kwanza cha mradi wa reli ya kisasa SGR Dar es Salaam -Morogoro reli zote za SGR zilizotumika katika ujenzi pamoja na mitambo mingine ilisafirishwa kwa kutumia behewa za wazi za MGR ambazo hata hivyo hazikutosheleza mahitaji kilingana na mizigo iliyoingia bandarini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!