Taasisi ya Diamonds in the Sky foundation wametoa msaada wa vifaa vya kusomea na michezo kwa wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Dovya iliyopo Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mbunge wa Temeke Mhe. Doroth Kilave na kusema kuwa watu wengine waige mfano wa vijana hao waliosoma kukumbuka nyumbani.
Aidha Kilave ameshukuru taasisi ya Diamond in the Sky foundation kwa kutoa msaada huo na kutaka taasisi nyingine kujitokeza kusaidia watu wenye uhitaji.
“Wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa sambamba na wazazi wanaoishi na watoto wenye ulemavu wawatoe siku ya sensa wahesabiwe “amesema Kilave.
Pia Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Jacqueline Lussa amesema wamefanya hivyo kwa kutambua uwepo wa watu wenye ulemavu katika jamii nao wanahitaji elimu na huduma nyingine za kijamii.
“Nawasihi wazazi wote ambao wanaishi na watoto wenye ulemavu nyumbani wawatoe nje ili wapate kuhesabiwa serikali itakapo pata takwimu sahihi iweze kutoa huduma kwa urahisi zaidi “amesema Lussa.
Sanjari na hayo Mkurugenzi Msaidizi Sondole Bulega amesema msaada huo waliotoa unalengo la kuhamasisha wadau wengine wajitokeze kuwasaidia watu wenye uhitaji iwe kwa makundi au mtu mmoja mmoja.
“Jamii wasione aibu walete watoto katika vituo wapate elimu na huduma kwani mtoto mwenye ulemavu anahaki ya kupata mahitaji muhimu kama watoto wengine ambao hawana ulemavu “amesema Bulega.