Home Kitaifa SHAKA ATOLEA UFAFANUZI MAADHIMIO AMBAYO YAMEFIKIWA KATIKA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU TAIFA

SHAKA ATOLEA UFAFANUZI MAADHIMIO AMBAYO YAMEFIKIWA KATIKA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU TAIFA

Na Magreth Mbinga

Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM ilipokea na kujadili taarifa mbalimbali juu ya utendaji wa Chama sambamba na utendaji wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikatoka na maadhimio ya Kumpongeza Mwenyekiti wa Chama hicho ambae ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamezungumzwa na Katibu wa Uenezi na Itikadi Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka katika kikao chake na Waandishi wa habari kilicholenga kutolea ufafanuzi juu ya maadhimio ambayo kamati imetokanayo September 7.

Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha anapunguza makali ya tozo ,kutoa ruzuku na mbolea kwa wakulima jambo ambalo limesaidia sana kuwafanya wakulima kutokuwa na hofu ya uwekezaji wao katika sekta ya Kilimo“amesema Shaka.

Pia Shaka amesema kwenye bajeti ya mwaka 2022-2023 katika sekta ya kilimo imetengwa Bilioni 954 sawa na 224% ya bajeti jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Nchi ya Tanzania ambapo fedha hizo zimeelekezwa kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima kwaajili ya kuongeza tija na kushusha bei ya pembejeo kwa wakulima na kujenga miundombinu ya umwagiliaji.

Kamati kuu imempongeza Rais Samia kwa kufanikisha sensa ya watu na makazi ya kidijitali kwa mara ya kwanza imempongeza kwa kutenga fedha na mipango mizuri ya kufanikisha sensa yenyewe kwa Watanzania“amesema Shaka.

Sanjari na hayo Kamati kuu imempongeza Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh Hussein Mwinyi kwa namana ambavyo ameendelea kusimamia uendeshaji wa Serikali ambayo inamfumo wa umoja wa Kitaifa na kuendelea kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo yenye dhamira ya kuwapunguzia Wananchi umasikiani pamoja na kuinua uchumi wa Zanzibar.

Dokta Mwinyi amefanya kazi nzuri sana na kamati kuu imeridhishwa na inampongeza kwa dhati hasa katika siku hizi za karibuni namna ambavyo ameonyesha uimara katika kuchukua hatua dhidi ya ufisadi uhujumu uchumi na rushwa ambapo tumeona tayari juhudi kadhaa zimeanza kuchukuliwa hasa baada ya kupokelewa kwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar” amesema Shaka.

Aidha Kamati kuu imeona umuhimu wa Serikali kusikiliza maoni na ushauri wa Wananchi kuhusu utekelezaji wa bajeti hiyo hususa katika eneo la tozo za miamala ya kielektroniki iliyoanza kutekelezwa hivi karibuni Kamati Kuu imeishauri Serikali kusikiliza maoni na ushauri wa Wananchi kuhusu swala zima la tozo.

Vilevile Kamati kuu imepokea maendeleo ya Mchakato wa Taifa wa kuwapata Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Chama kinaendelea na utaratibu wa ndani endapo utaratibu utakapo kamilika Chama kitatoa taarifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!