Home Kitaifa SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA WADAU FURSA ZA KIDIGITALI

SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA WADAU FURSA ZA KIDIGITALI

Na Mwandishi wetu, MzawaOnline

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa Sekta binafsi katika kukabiliana na tatizo la ajira nchini Tanzania ikiwemo kuwajengea uwezo na uwelewa vijana juu ya fursa za kiditali katika mabadiliko ya matumizi ya Tehama huku ikiahidi kuweka sera wezeshi na rariki katika kuwafikia vijana wengi.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam nsma Naibu Waziri wa Wizara ya Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya habari Kundo Mathew wakati akifungua Jukwaa la Kidigitali kwa Maendeleo ya vijana ambapo amesema tatizo la ajira bado ni changamoto na Serikali haiwezi kuajiri watu wote, hivyo lazima washirikiane na wadau mbalimbali katika kutatua tatizo la ajira.

Serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi tumeamua kuwajenga uwelewa Vijana kwa namna ya kufanya fursa za Kidigitali katika Mabadiliko ya Tehama kuwa sehemu ya fursa za kibiashara na kujikwamua kiuchumi kwani Serikali haiwezi kuajiri watu wote nchini“amesema Naibu Waziri Kundo.

Aidha, amesema Serikali imeweka sera wezeshi itakayosaidia vijana kupata ajira kwa njia ya mitandao ikiwemo kutengeneza matumizi au programu zitakazotumiwa katika mifumo ya kibiashara na matumizi kwa jamii na hatimae kuweza kujiajiri wenyewe na kupunguza wimbi kubwa la vijana ambao hawana ajira.

Kupita jukwaa la Kongamano la vijana wa Kidigitali wapatao 2500 kutaweza kurahisisha upatikanaji wa program mbalimbali pamoja na fursa za ajira kutoka ndani na nje ya nchi hivyo tutaweza kupata wataalam wapya katika taifa letu “amesema Naibu Waziri Kundo.

Hata hivyo, amesema kuwa Serikali inaandaa mchakato wa kutunga sera itakayoweza wataalam wote wapya wa program mbalimbali kupewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao Ili kutambulika kwa haraka na kupata fursa Kimataifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama, Nkundwe Mwasaga amesema tume ya tehama inahakikisha inatumia Vijana kuwasaidia kujenga ueleewa katika fursa za Kidigitali pamoja na kuwakuza katika tehama.

Sio kuwajenga tu ueleewa bali itahakikisha inafungua milango ya fursa na kuwakuza bila kujali Elimu yao ili kutengeneza wataalam ambao watakua wazuri kutangaza taifa letu katika Mabadiliko hayo mapya ya tehama katika fursa za Kidigitali na kutegemea uwekezaji mpya kutokana na fursa hizo“.

Naye, Meneja Mawasiliano na ushirikiano kutoka Taasisi ya fursa za Kidigitali (DOT) Ndimbumi Msongole amesema Taasisi hiyo inahakikisha vijana wanapata fursa bila kujali wametoka maeneo yapi kuanzia mjini hadi vijijini hususani kwenye sehemu zinazopata mkongo wa taifa kwa uzuri zaidi.

Aidha, amesema kuwa kwa sasa takribani mikoa 11 imekua nufaika na jukwaa la fursa za kidigitali na maendeleo kwa vijana lengo ni kusaidia vijana pamoja na Serikali kuwezesha upatikanaji wa ajira kwa haraka zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!