Home Kitaifa SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO SEKTA YA KILIMO

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO SEKTA YA KILIMO

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kuhakikisha inatatua changamoto zinazokabili sekta hiyo ili kuwawezesha wakulima kufanya kilimo kinachoendana na teknolojia kitakachosaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuchangia pato la Taifa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Kilimo Bwa. Joseph Kiraiya wakati akiongoza kikao cha majadiliano kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kuhusu Mkakati wa Nchi wa AGRA TANZANIA katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

Mkurugenzi huyo alisema Programu ya kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ni mpango wa miaka 10 unaolenga kuleta mageuzi ya sekta ya kilimo (Kilimo, Mifugo na Uvuvi), kuongeza uzalishaji wenye tija na kufanya kilimo kuwa cha kibiashara.

“Mpango huu nia yake ni kuleta mageuzi kwa sekta hii kama tunavyojua ina mchango mkubwa sana katika pato la Nchi yetu hata wakulima kipato chao kitaongezeka, tutakuwa na chakula cha kutosha, usalama wa chakula na lishe,” alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha Makamu wa rais anayesimamia Sera kutoka Shirika la Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) Dkt. Nwafor Apollos alibainisha kwa shirika hilo liko tayari kufanya kazi na serikali katika kuboresha mazingira ya kilimo nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!