Home Kitaifa WAZIRI BASHUNGWA AIPONGEZA NYAISHOZI SEKONDARI KUINGIA 10 BORA KITAIFA MATOKEO YA KIDATO...

WAZIRI BASHUNGWA AIPONGEZA NYAISHOZI SEKONDARI KUINGIA 10 BORA KITAIFA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mbunge wa Jimbo la karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa ameipongeza shule ya Sekondari Nyaishozi iliyopo wilayani Karagwe mkoani Kagera kwa kufanya vizuri katika matokeo ya mtiani wa kidato cha sita mwaka 2022 na kushika nafasi ya saba kitaifa.

Ametoa pongezi hizo Julai 14, 2022 alipotembelea shule hiyo na kupata fursa ya kuongea na wanafunzi, walimu na uongozi wa shule hiyo inaomilikiwa na Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Karagwe na Kyerwa (KDCU).

Bashungwa amesema matokeo mazuri katika shule hiyo yamechangiwa na kazi kubwa ya kujituma ya walimu na watumishi wa shule hiyo na utayali wa wanafunzi kujifunza katika mazingira mazuri na wezeshi yaliyowekwa na uongozi wa shule.

Amesema uwekezaji wa taasisi ya shule ya Nyaishozi ni mfano mzuri wa namna ya kutumia ushirika.

Pia amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuboresha ushirika ili uweze kumsaidia mkulima mdogo mdogo kwa kipato kinachotokana na kuongezeka kwa bei ya kahawa.

Aidha, Bashungwa ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wanafunzi wa kidato wa kidato cha kwanza hadi cha sita kwa kuwasihi kuendelea kuelekeza akili yako katika masomo maana Wao ndio wanategemewa kuwa wataalamu na viongozi wazuri katika miaka ijayo.

Ameuhakikishia uongozi wa shule kuwa Serikari itaendelea kushirikiana na shule hiyo ili kuhakikisha mafaniko yaliyopatikana mwaka huu yanendelezwa kwa miaka mingine.

Naye, Mkuu wa Shule ya Nyaishozi, Mwalimu Audax Gereon amesema Shule ya Sekondari Nyaishozi ilianzishwa mwaka 1990 na ina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita kwa mchanyanyiko wa wavulana na wasichachana na wote wanaishi shuleni.

Amesema matokeo mazuri ya Mwaka 2022 ni mwendelezo wa matokeo mazuri ya miaka ya nyuma ambapo mwaka 2020 shule ilishika nafasi ya 17 kitaifa, vilevile mwaka 2021 shule ilishika nafasi ya 11 kitaifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!