Home Kitaifa SERIKALI INATARAJIA UWEKEZAJI HUU KUWAGUSA MOJA KWA MOJA WANANCHI WA WILAYA YA...

SERIKALI INATARAJIA UWEKEZAJI HUU KUWAGUSA MOJA KWA MOJA WANANCHI WA WILAYA YA MKINGA, MKOA WA TANGA NA NCHI KWA UJUMLA

Serikali kupitia wizara ya Uwekezaji,viwanda na Biashara imezitaka kampuni na mashirika ya nje na ndani ya nchi yanayotaka kuwekeza Nchi kuzigatia utunzaji wa mazingira kwa Kuja na teknlojia ya kisasa itakayo wezesha kuendelea kuweka mazingira salama kwaajili ya kuvutia wawekezaji wengine zaidi.

Hayo yalisemwa jana Jijini Dar Es Salaam na Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Exaud Kigahe wakati wa Uzinduzi Rasmi wa Mradi wa kanda maalum ya Kiuchumi ya Mkinga.,ambapo alisema Sekta binafsi ni moja ya sehemu kubwa kwa serikali katika kuakikisha uchumi wa nchi unakua.

Akizungumzia Uzinduzi huo wa Kanda maalum ya Kiuchumi ya Mkinga, Waziri Kihage aliwapongeza wawekezaji hao kwa kuziona fursa zilizopo mkoani Tanga na kisisitiza kuwa serikali itawaunga mkono kwa kuwezesha uwekezaji huo kuwa na tija kwa kwao na kwa serikali.

Serikali inatarajia uwekezaji huu kuwagusa moja kwa moja wananchi wa wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga na Nchi kwa ujumla kwani hiyo ndio itakuwa njia sahihi ya kuukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na hivo kuleta Tija katika uchumi wa Taifa” Alisema Kigahe

Alisema takribani zaidi ya ajira rasmi 300 na zisizokuwa rasmi zinatarajiwa kuzalishwa kwenye Mradi huo na utekelezaji wake utakuwa ni wa kiwango cha kimataifa.

Mradi huo unatarajiwa kuwa na eneo la ofisi,ghala la kuntena,kituo cha mikusanyiko,kituo cha gesi,makazi ya familia na wafanyakazi,kituo cha matibabu pamoja na Hotel.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mkinga Economic Zone Ally Kassim alisema lengo la Mradi huo ni kutekeleza maagizo ya serikali katika kuakikisha uwekezaji nchini unaongezeka hususani katika maeno yote nchini ili kuleta usawa wa kiuchumi katika maeneo utakaofanyia uwekezaji husika.

Rais Samia na serikali kwa ujumla inapenda kuona uwekezaji unakuwa na kuongezeka kote nchini,na sisi lengo letu ni kuhakikisha tunalitimiza ilo ili Nchi izidi kusonga mbele ” Kassim alisema

Wawekezaji hao wamethibitisha kuwa hadi sasa jumla ya wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali wameonyesha nia ya kuwekeza fedha zao ikiwa ni pamoja na Nchi ya Brazil, Misri, Tunisia, Bulgaria, GCC, Ufilipino Na India.

Nae mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba Alisema wawekezaji huo hawajaja bahati mbaya kwani Mkoa huo una fursa nyingi ambazo wao wameziona ikiwa ni pamoja na Bandari,Bomba la mafuta pamoja na Ardhi yenye rutuba ,na kuongeza kuwa itawarahisishia katika kusafirisha bidhaa na vitendea kazi kutoka ndani na nje ya nchi kwa urahisi ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani katika malighafi na mazao.

Mradi huo wenye thamani ya Dola Milioni 300 sawa na Shilingi Bilioni 699 unatarajiwa kuleta Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika kutokana na kuambatana na teknolojia za kiwango cha kimataifa ikiwa ni pamoja na teknolojia ya akili bandia ( Artificial Intelligence ), Biashara ya mtandao hivo kufanya kuwa Mradi wa kipekee.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!