Home Kitaifa RC MGUMBA AWATAKA WAHITIMU JKT KUJIEPUSHA NA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA...

RC MGUMBA AWATAKA WAHITIMU JKT KUJIEPUSHA NA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII.

NA BONIFACE GIDEON,HANDENI

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa Nchini Operesheni Venancy Mabeyo 2022 wanaokwenda kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini kutumia vizuri mitandao ya kijamii badala ya kutumia kwenye mambo ya kuweka picha za utupu ambazo zimekuwa zikiwadhalilisha na kuleta fedheha kwa Taifa .

Mgumba ameyasema hayo wakati akifunga leo mafunzo katika kambi ya JKT Kabuku 835 KJ wilayani Handeni Mkoani Tanga ambapo alisema vijana wengi waliopo vyuoni wamekuwa na uhuru uliopitiliza na kufanya mambo bila uwepo wa usimamizi.

Aidha Mgumba amewataka vijana hao wasiende kuwa na uhuru uliopitiliza na kuwasisitiza kuwa na nidhamu katika matimizi mazuri ya mitandao ya kijamii kwajili ya kujipatia faida.

Alisema lazima wazazi washirikiane katika kuwatembelea watoto wao mara kwa mara kwa maana unaweza kujua mtoto wako anasoma kumbe anasomeshwa jambo ambalo baadae linaweza kuwa na athari kwake na Jamii kwa ujumla.

“Niwasihi wazazi wenzangu muwe mnafanya kuwatembelea watoto wenu wanapokuwa vyuoni lakini wahitumu leo niwaase mkatumie vizuri mitandao ya kijamii kwa ajili ya faida na sio vinginevyo maana vijana wengine waliopo vyuoni wanaweza kudanganywa kwenye mitandao ya kijamii ukashurutishwa jambo ambalo unaweza kufanya kwa tamaa”Alisema

Mkuu huyo wa Mkoa alisema matokeo yake wanadhalilisha wazee wao Jamii na Ndugu na Taifa kwa ujumla hivyo hakikisheni suala la nidhamu wanalishikilia kweli hasa wale wanaoenda kuishi vyuoni.

“Kwa sababu mtakumbana na watu mbalimbali ikiwemo wanasheria wasije kuwapotosha nyie mmeiva na mmefundwa nidhami na uadilifu kaishini maisha hayo”Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Awali akizungumza wakati wa ufunguji wa mafunzo hayo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele aliwataka wahitimu wa mafunzo wasiende kutu mika vibaya katika maeneo mrakayokuwepo wakati wote mkumbuke kiapo mlichoapa.

Alisema kuwa kama wanavyofahamu majukumu ya JKT ni malezi ya vijana na uzalishaji wa mali na kufanya shughuli za ulinzi wa Taifa katika kutekeleza majukumu hayo ya kila siku.

Hata hivyo alisema hivyo kutolewa mafunzo hayo kwa vijana wa mujibu wa sheria na mafunzo ya mujibu wa sheria Op Jenarali Mabeyo yamekuchukua uda majuma 12 mfululizo.

Mkuu wa JKT alisema kwamba wahitimu hao wamejifunzamasomo mbalimbi yakiwemo ya uzalishaji mali,nadharia na vitendo kwa ujumla lengo kukuza moyo wa uzalendo kuwajengea nidhamu ,ukakamavu na ujasiri.

Alisema hiyo itawafanya wajitambue kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuilinda,kuijenga na kuitetea nchi yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha 835 KJ JKT Kabuku Luteni Kanali Raymond Mwanri alisema vijana hao wakiwa kwenye mafunzo hayo wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo ulinzi wa Taifa lao,Uzalendo na utii kwa mamlaka zilizowekwa kwa mujibu wa sheria .

Hata hivyo aliwataka wahitimu hao kuhakikisha wanakiishi kiapo hicho huku akieleza wamefaulu katika viwango mbalimbali vya kuhitimua mafunzo hayo.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!