Home Kitaifa MWIGOBERO FC YATINGA NUSU FAINALI POLISI JAMII CUP MUSOMA KWA KISHINDO

MWIGOBERO FC YATINGA NUSU FAINALI POLISI JAMII CUP MUSOMA KWA KISHINDO

Na Shomari Binda-Musoma

TIMU ya Mwigobero fc imetinga hatua ya nusu fainali kwa kishindo baada ya kuifunga timu ya Musoma Boys mabao 5-1 kwenye mfululizo wa michezo ya Polisi Jamii Cup 2024 Musoma

Mwigobero imetinga hatua hiyo ikitokea kundi B na hivyo kusubili mpinzani wake atakayetoka kundi A.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo uliofanyika septemba 20 kwenye uwanja wa Mara sekondari,kocha wa timu ya Mwigobero Richard Leuben amesema anawapongeza wachezaji wake kwa kufuata maelekezo na kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Amesema mchezo ulikuwa mgumu kwa kuwa walikuwa wakihitaji ushindi na mabao 3 lakini walifanikiwa kufikisha 5.

Richard maarufu kama ” Wa Mkoa”amesema wanajipanga na kufanya maandalizi ya mchezo wa nusu fainali waweze kufanya vuzuri na kuingia fainali baadae wachukue ubingwa.

Kwa upande wake kocha wa Musoma Boys Zamoyoni Taruma ambaye timu yake imeishia hatua ya makundi amesema hawakucheza vizuri kwenye mchezo huo na wanakwenda kujipanga na mashindano mengine.

Mmoja wa waratibu wa mashindano hayo Omary Girbert amesema ushindani umekuwa mkubwa kwenye michezo ya mwisho hatua ya makundi.

Amesema hatua hiyo itahitimishwa siku ya jumatatu kabla ya michezo ya nusu fainali na fainali itaayofanyika septemba 30

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!