Home Kitaifa MKANDARASI ATAKIWA KUMALIZA BARABARA KWA WAKATI/ WANANCHI WACHEKELEA SASA

MKANDARASI ATAKIWA KUMALIZA BARABARA KWA WAKATI/ WANANCHI WACHEKELEA SASA

Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Muleba mkoani Kagera imeagiza Barabara zote zinazotekelezwa wilayani humo kukamilika kwa wakati na kuzingatia ubora unaotakiwa.

Kamati hiyo imetoa maagizo hayo Agosti 31 Mwaka huu wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Barabara inayosimamiwa na Tarura chini ya katibu tawala wa Wilaya hiyo Greyson Mwengu.

Greyson amesema kuwa katika ziara hiyo kamati ya ulinzi umeamua kutembelea Barabara Nne ambazo zinajengwa kwa garama ya shilingi bilioni 1.3 nakuongeza kuwa maagizo ya wilaya ni kuona miradi hiyo inakamilikaa kw amuda uliopangwa pasipo na nyongeza ya Muda.

Kwa upande wake kaimu meneja wa Tarura wilaya ya Muleba amesema kuwa Barabara hizo zinajengwa na wakandarasi wawili tofauti na kusema kuwa pesa za utekelezaji wake zinatoka mfumo wa Barabara.

Ameongeza kuwa hadi sasa utekelezaji wa miradi hiyo umefikia asilimia 30% ambapo utekelezaji ulianza Julai Mwaka huu na inatakiwa kukabithiwa Disemba Mwaka huu.

Waliongea kwa nyakati tofauti Wananchi ambao ni watumiaji wa Barabara hizo wameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuwafungulia barabara ambazo zilikuwa zikiwapa tabu sana hasa nyakati za mvua na kufanya kutokuwepo kwa mawasiliano katika maeneo mbalimbali.

Wameeleza kuwa changamoto ya kushindwa kupeleka mazao Yao sokoni inakwenda kumalizika maana Barabara zilikuwa kikwazo kikubwa katika kulifikia hilo ambapo wanasema inabaki kuwa HISTORIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!