Waziri wa Nchi Afisi ya Rais – Kazi, Uchumi na Uwekezaji,Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga Ameshiriki katika kongamano la majadiliano ya namna ya kuwavutia wawekezaji wa Mitaji Binafsi barani Afrika kwa kuzingatia athari za janga la ugonjwa wa Uviko-19, mabadiliko ya tabia Nchi na mienendo ya uchumi na biashara duniani, linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hayatt Regency jijini Daresalam tarehe 14-15 Septemba 2022.
Kongamano hilo limejumuisha viongozi mbali mbali wa Serikali za Afrika wanaohusika na masula ya Fedha na Uwekezaji kutoka Nchi 21, taasisi ya MIGA pamoja na wawekezaji wakubwa katika sekta mbali mbali ikiwemo Sekta ya Kilimo, Nishati, Mawasiliano, Miundombinu, Maji, Viwanda, Utalii na taasisi za Kifedha.