Home Burudani MASHINDANO YA INSTAQUEEN KUFANYIKA DESEMBA 5, 2023; MABINTI CHANGAMKENI

MASHINDANO YA INSTAQUEEN KUFANYIKA DESEMBA 5, 2023; MABINTI CHANGAMKENI

Na Magrethy Katengu

Fursa zaibuka kwa mabinti kupitia mtandao wa Instagram katika mashindano InstaQeen ya kutuma video na picha zao vigezo na Masharti kuzingatiwa Zawadi nono Pesa taslimu kutolewa katika mashindano ya Instaqueen yatakayofanyika Disemba 5, 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 20, 2023 jijini Dar es Salaam Balozi wa wa mashindano hayo Meena Ally amesema weandaa Mashindano vigezo ikiwa ni unadhifu kujiamini huku umri ni kuanzia wa miaka 18- 35 ambapo watatuma video na picha kupitia namba +258842555649 na Majina yao matatu ikiambatanishwa na namba ya Nida hivyo mabinti wote Tanzania popote walipo watumie fursa hiyo adhimu haiangalii Elimu cha msingi ni kujiamini .

“Tumejipanga vizuri Mashindi wa kwanza atapatiwa zawadi ya shilingi milioni 3, wapili shilingi milioni 2, watatu shilingi milioni 1 na wote watapatiwa kazi za kudumu wengine furasa ya kusoma au kuendeleza kipaji alichonacho kwani tunaamini wapo wenye vipaji lakini changamoto fedha ya kujiendeleza kiwe fursa” amesema Meena Ally

Sambamba na hayo Instaqueen ni mashindano ya urembo ya kidigitali ya kwanza Tanzania ambayo yanasherehekea uzuri, vipaji, na ufanisi kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii, haswa Instagram, washiriki wanatuma picha tatu na video zao full na fupi wakijielezea wasifu wao pamoja na ujumbe wa kuomba kujiunga na Instaqueen Tanzania.

Mtu yeyote anayekidhi vigezo na masharti ya Instaqueen anaruhusiwa kushiriki mashindano ya Instaqueen, ikiwemo kigezo cha umri wa miaka 18-35, uraia wake awe Mtanzania, awe Mwenye maadili na picha zake ziwe za kimaadili unadhifu utaangaliwa

Amesema Instaqueen ilizaliwa kwa nia ya kutoa au kutengeneza jukwaa kwa watu kuonyesha uzuri na vipaji vyao pekee kidijitali, kwamba lengo lake ni kuwapa fursa watu walio wengi ambao wanatamani kutambulisha na jamii, kuwa watu maarufu na kuonyesha vipaji vyao.

Kwa upande wake Dkt. Kumbuka ambaye ni Balozi mwengine wa Mashindano hayo yanalenga kubadilisha mawazo ya Vijana katika kutumia mitandao ya kijamii kwa maendeleo chanya kwao na kwa jamii inayomzunguka.

Kwamba inawasaidia washindani kujiamini, kuendeleza vipaji vyao katika tasnia ya urembo, kujifunza mengi kuhusiana na masuala ya urembo, na kupata kutambuliwa katika tasnia ya urembo na mitindo na cha pili Instaqueen inatoa fursa za Kazi na kuongeza ujuzi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mashindano ya InstaQueen Tanzania Maximilian Donald amesema Instaqueen ina raundi ambazo ni pamoja na utumaji maombi na kupokelewa kwa maombi, mchujo kupitia kura za wananchi ambayo ni hatua ya mtoano, kisha Nusu fainali na baadaye fainali yenyewe.

Donald ameeleza kwamba Instaqueen inatumia nguvu ya mitandao ya kijamii, ikifanya iweze kupatikana kwa hadhara ya ulimwengu.

Aidha Wazazi walezi ndugu jamaa na marafiki ambao hawana simu janja na wanapenda kushiriki Binti yao wamwazime simu atume picha na video zake huku akiweka mawasiliano yake ili akitafutwa apatikane kwa urahisi zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!