Home Kitaifa KISARAWE KUNUFAIKA NA KILOMITA 34.5 ZA BARABARA ZA LAMI: DKT. JAFO AMUOMBA...

KISARAWE KUNUFAIKA NA KILOMITA 34.5 ZA BARABARA ZA LAMI: DKT. JAFO AMUOMBA WANANCHI KUMPA NAFASI TENA

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kisarawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Seleman Jafo, ameendelea kuwataka wananchi wa jimbo hilo kumpa ridhaa ya ndiyo ili aendelee kuwatumikia, huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

Akizungumza Septemba 06, 2025, Dkt. Jafo alisema Rais Samia ndiye kiongozi wa kwanza kutangaza kwa mara moja ujenzi wa kilomita 34.5 za barabara za lami ndani ya Kisarawe, jambo ambalo linaonyesha dhamira ya dhati ya serikali kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Kwa mara ya kwanza, Rais Samia ametangaza kilomita 34.5 za barabara, jambo linalothibitisha nia ya kweli ya kuhakikisha Kisarawe inafunguka kimaendeleo. Hii ni heshima kubwa kwa wananchi wetu,” alisema Dkt. Jafo.

Aidha, alisema Rais Samia amehakikisha miradi yote yenye thamani kubwa ya fedha imepatiwa ufumbuzi wa kifedha ili ikamilike kwa wakati.

Akifafanua ajenda yake binafsi, Dkt. Jafo alisisitiza kuwa kipaumbele chake ni barabara, ili kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Kisarawe, huku akiendelea kuimarisha sekta nyingine muhimu kama afya, elimu, maji na umeme vijijini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!