Home Michezo HAJI MANARA AJIUNGA NA PARIMATCH

HAJI MANARA AJIUNGA NA PARIMATCH

KAMPUNI ya Ubashiri nchini Parimatch imemtangaza Mwanaharakati Haji Manara kama Balozi mpya wa Kampuni hiyo ili kuitangaza vizuri ndani na nje ya nchi Kampuni hiyo na bidhaa zake.

Akizungumza mapema leo Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Levis Paul amesema hawajafanya Makosa kumchagua Haji Manara kuwa balozi wao kwani wanatambua nafasi na wafuasi wengi alionao ambao wamekuwa wakimfatilia katika mitandao ya kijamii pamoja na shughuli za kimichezo alizokuwa akifanya hapo awali.

“Kampuni zote za Kisasa ambazo zinafanya biashara kipindi hiki zinalazimika kutafuta njia mbadala za kukuza ufahamu wa chapa zao (brand) sisi kama Parimatch tunaamini na tunatambua nguvu kubwa uweledi wake Haji Manara katika kukuza chapa za Kampuni mbalimbali”

Levis pia ameongeza kuwa wamejiridhisha kiutafiti kuwa anaweza kuisemea Kampuni vizuri na sura ya chapa ya Parimatch nje na ndani ya nchi.

Kwa upande wake Balozi huyo Mpya wa Kampuni ya Parimatch Haji Manara ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha Kampuni hiyo inafika malengo waliojiwekea.

Hata hivyo amesema anatambua kuwa Kampuni za ubashiri zipo nyingi na kwa sasa zimekuwa za ushindani hivyo atatumia maarifa yake na uwezo wake kupitia ushindani huo huo Kampuni inafikia wateja wake na kutambulika zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!