Home Michezo GEKUL AWAPA MABALOZI MKAKATI WA KUBIDHAISHA KISWAHILI

GEKUL AWAPA MABALOZI MKAKATI WA KUBIDHAISHA KISWAHILI

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amekutana na Mabalozi watatu wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Zambia, Zimbabwe na Uholanzi ikiwa ni hatua ya kuimarisha na kuendeleza lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania.

Akiongea na Mabalozi Mhe. Simon Sirro Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Caroline Chipeta Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi na Mhe. Luteni Generali Mathew Mkingule Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Ofisini kwake Mtumba Mji wa Serikali jijini Dodoma Septemba 20, 2022, Naibu Waziri Mhe. Gekul aliwataka Mabalozi hao kusimamia na kueneza lugha ya Kiswahili kwenye nchi walizopangwa kwa kuwa sasa lugha ya Kiswahili inatumika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Umoja wa Afrika na Duniani kote.

Viongozi hao walikabidhiwa vitabu vya kufundishia lugha ya Kiswahili ikiwemo Kamusi Kuu ya Kiswahili Toleo la Tatu la 2022, Mwongozo wa Kufundisha Kiswahili kwa Wageni pamoja na kitabu cha Furahia Kiswahili ambavyo vyote ni nyenzo za kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili katika nchi wanazokwenda kufanyakazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!